Ashura inaadhimisha kumbukumbu ya kuuawa shahidi Imam Hussein (AS), na rangi nyekundu inaashiria kifo cha kishahidi.
Haidar al-Issawi, afisa wa Astan (ulezi) wa hekalu takatifu huko Najaf, alisema zaidi ya mita za mraba 25,000 za ua zimefunikwa na zulia jekundu.
Amesema mpango jumuishi umetekelezwa katika kaburi la Imam Ali (AS) ili kuwakaribisha waombolezaji katika siku kumi za mwanzo za mwezi wa Hijri wa Muharram.
Aliongeza kuwa zaidi ya vibanda 100 vya Moukeb (vibanda vya kutoa chakula na vinywaji kwa wafanya ziyara vimeanzishwa kwa ajili ya kuwahudumia wafanya ziyara.
Astan imewapa Moukeb kiyoyozi na kutoa maji ya kunywa, sabuni, nk, alisema.
Kulingana na al-Issawi, Astan inataka kuwapa wafanya ziyara na waombolezaji huduma bora zaidi.
Madhehebu Tukufu ya Imam Hussein (AS) yakitayarishwa kwa Ibada ya Rakdha Tuwairaj
Muharram ni mwezi wa kwanza katika kalenda ya mwandamo ya Hijri.
Waislamu wa madhehebu ya Shia na wengineo katika sehemu mbali mbali za dunia hufanya maombolezo kila mwaka katika mwezi wa Muharram kuomboleza kumbukumbu ya kuuawa shahidi Imam Hussein (AS) na masahaba zake.
Imamu wa tatu wa Shia (AS) na kikundi kidogo cha wafuasi wake na wanafamilia wake waliuawa kishahidi na dhalimu wa zama zake - Yazid Bin Muawiya, katika vita vya Karbala katika siku ya kumi ya Muharram (ijulikanayo kama Ashura) mwaka wa 680. AD.