Rais Masoud Pezeshkian amesema hayo hapa mjini Tehran katika Kongamano la 38 la Kimataifa la Umoja wa Kiislamu lililohudhuriwa na wanafikra na wanazuoni kutoka nchi mbalimbali za Kiislamu, na kusisitiza kwamba, ni lazima tushikane mkono, umoja na mshikamano wa sisi Waislamu unaongeza nguvu zetu.
Rais Pezeshkian ameongeza kuwa, Israel inatenda jinai kwa sababu hatuna maono na lugha moja sisi kwa sisi, hatuna umoja wa Kiislamu, tunapigania mambo mepesi, Sala na saumu ni kwa ajili ya umoja, kama hamna umoja baina yenu mnafunga na kuswali kwa ajili ya nini?
Mkutano wa 38 wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu unaofanyika chini ya kaulimbiu "Ushirikiano wa Kiislamu ili Kufikia Thamani za Pamoja kwa Kutilia Mkazo Suala la Palestina" umeanza hapa Tehran kwa kuhudhuriwa na wageni 2,500 mbalimbali wakiwemo shakhsia wa kijeshi na pia wasomi na wanafikra wa nchi za Kiislamu.
Siku ya 17 ya Rabiul Awwal, ambayo ni Septemba 21 mwaka huu, inaaminika na Waislamu wa madhehebu ya Shia kuwa siku ya kukumbuka kuzaliwa kwa Mtume Mohammad (SAW), wakati Waislamu wa Sunni wanaamini tarehe sahihi ni 12 Rabiul Awwal
Muda kati ya tarehe hizo mbili huadhimishwa kila mwaka kama Wiki ya Umoja wa Kiislamu.
Hayati Mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Imam Khomeini (RA) ndiye alitangaza muda baina ya tarehe hizo mbili kuwa Wiki ya Umoja wa Kiislamu nyuma katika miaka ya 1980.
3489962