Mapema leo Jumatano, watu wenye silaha wasiojulikana walifyatua risasi sambamba na kuvurumisha roketi za RPG na maguruneti kwenye jengo hilo, kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwenye kituo cha Telegram cha ofisi ya mwanazuoni huyo.
Mmoja wa walinzi wa mwanazuoni huyo mkuu anasemekana kujeruhiwa katika shambulio hilo, tovuti ya Al-Sumaria News iliripoti.
Hakuna aliyedai kuhusika na shambulio hilo.
4245189