IQNA

Harakati za Qur'ani

Wahifadhi wa Qur'ani wa Algeria wazawadiwa safari ya Umrah

13:50 - November 28, 2022
Habari ID: 3476162
TEHRAN (IQNA) – Algeria imewazawadia safari Umrah kwa wanafunzi 168 wa vyuo vikuu ambao wamefanikiwa kuhifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu..

Katika hafla iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Oran 1 Ahmed Ben Bella, huko Oran, kaskazini-magharibi mwa Algeria, maafisa wa nchi hiyo wamewaenzi makumi ya wanafunzi wa kiume na wa kike ambao wameweza kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu.

Kwa mujibu wa taarifa, hii ilikuwa sherehe kubwa zaidi ya aina yake ya kuwaenzi waliohifadhi Qur'ani Tukufu  katika vyuo vikuu vya Algeria.

Al-Saeed Saoud, gavana wa Oran, aliwatunuku wanafunzi 168 tuzo zilizojumuisha tikiti za kwenda Saudi Arabia kwa ajili ya Hija Ndogo ya Umrah.

Kikiwa na wahifadhi Qur'ani 60, kitivo cha matibabu cha Chuo Kikuu cha Oran kilisajili idadi kubwa zaidi ya wanafunzi waliotunukiwa zawadi katika hafla hii.

Wanafunzi wengine walitoka katika vyuo vya sayansi za jamii, dawa, na udaktari wa meno.

Algeria ni nchi ya Kiarabu iliyoko Afrika Kaskazini. Waislamu ni takriban asilimia tisini na tisa ya wakazi wa nchi hiyo.

4102938

Kishikizo: algeria ، qurani tukufu ، waislamu
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha