IQNA

Muqawama

Mkutano wa Kimataifa wa  'Fikra Nasrallah' Kufanyika Tehran

15:59 - November 03, 2024
Habari ID: 3479691
IQNA - Mji mkuu wa Iran, Tehran, utakuwa mwenyeji wa mkutano wa kimataifa wiki ijayo kujadili fikra za Katibu Mkuu wa zamani wa Hizbullah, Shahidi SayyidHassan Nasrallah.

Mkutano huo unaoitwa "Fikra za Nasallah", unaandaliwa na Shirika la Iran la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu (ICRO) mnamo Novemba 9, ikiwa ni siku ya 40 baada ya kuuawa shahidi mwanajihadi huyo.

Mkuu wa ICRO Hujjatul-Islam Mohammad Mehdi Imanipour alitangaza hayo na kuongeza kuwa mkutano wa wawakilishi kutoka vyombo tofauti vya kiutamaduni na kidiplomasia vya Iran hivi karibuni uliandaliwa ili kuratibu maandalizi ya mkutano huo.

‘School of Nasrallah’ Int’l Conference Slated for Nov. 9  

Alisema wageni 20 wa kigeni wametangaza utayari wa kushiriki katika hafla hiyo ya kimataifa.

Amemtaja Shahidi Nasrallah kuwa mtu mkubwa ambaye hatasahaulika katika historia ya muqawama yaani Mapambano ya Kiislamu, akisisitiza haja ya kuwepo ushirikiano wa vyombo vyote vinavyohusika ili kuufanya mkutano huo kuwa mkubwa kadiri inavyowezekana.

Wakati huo huo, Abbas Khameyar, katibu wa mkutano huo amemtaja Shahidi Nasrallah kuwa shakhsia  mkubwa Zaidi katika vita dhidi ya Uzayuni katika historia ya muqawama.

Aidha amebainisha kuwa wasomi na wanafikra kutoka Bahrain, Lebanon, Algeria, Iraq, Misri, Malaysia, Uturuki, Palestina, India, Yemen na Syria watashiriki katika hafla hiyo ya kimataifa.

Sayed Hassan Nasrallah aliuawa shahidi katika shambulizi kubwa la anga ambalo Israel ilitekeleza kusini mwa Beirut mnamo Septemba 27 kwa kutumia mabomu ya kivita yaliyotolewa na Marekani.

3490529

Habari zinazohusiana
captcha