IQNA

Muqawama

Mchambuzi wa Iraq asisitiza uthabiti wa muqawama katika mapambano na Israel

17:48 - October 05, 2024
Habari ID: 3479542
IQNA - Mchambuzi wa masuala ya kisiasa wa Iraq amewataka wapiganaji wa harakati za muqawama (mapambano ya Kiislamu) kuwa imara na wavumilivu katika makabiliano yao na utawala haramu wa Israel.

Akizungumza na Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA), Juma al-Atwani amesema wakati mhimili wa muqawama unakabiliwa na hali ngumu kwa kuzingatia yale yaliyojiri nchini Lebanon na Palestina hivi karibuni, wapiganaji  wa muqawama wanapaswa kukumbuka kuwa uthabiti, ushujaa na ustahimilivu ndio silaha zao kuu dhidi ya utawala ghasibu wa Israel.

Amesema wapiganaji wa muqawama wanapaswa kutumia nguvu zao zote na kuimarisha ari yao katika mapambano dhidi ya utawala huo unaokalia ardhi za wengine kwa mabavu.

Iwapo wataendelea kuwa na nguvu, adui wa Kizayuni atahisi kudhoofika na kushindwa kudhoofisha umoja wa mbele ya muqawama, amesema.

Al-Atwani ameashiria kuuawa shahidi hivi karibuni kwa Katibu Mkuu wa Hizbullah, Sayed Hassan Nasrallah na kusema alikuwa shujaa na jasiri.

Alisema kuwa kifo cha kishahidi kilikuwa ndoto ya Nasrallah tangu ujana wake na ndoto yake hatimaye ilitimia katika miaka yake ya 60.

Akifafanua vipengele tofauti vya shakhsia ya mkuu wa Hizbullah, amesema Nasrallah alikuwa amefungamana kikamilifu na Qur'ani Tukufu na alitiwa moyo na mafundisho ya Imam Hussein (AS) katika kukabiliana na dhulma, ukengeufu na ukandamizaji.

Alikuwa mtu mnyenyekevu wakati akimuomba Mwenyezi Mungu na kamanda jasiri na wa kipekee kwenye uwanja wa vita, al-Atwani alisema.

Kwingineko katika matamshi yake, mchambuzi huyo wa Iraq vita vya hivi sasa dhidi ya wavamizi wa Kizayuni huko Kusini mwa Lebanon ni hamasa kihistoria ambayo wapiganaji wa muqawama wanaibua.

Vile vile amesisitiza nafasi ambayo nchi za Kiislamu zinaweza kuchukua katika vita dhidi ya utawala wa Tel Aviv, akisikitika kwamba baadhi ya mataifa ya Kiarabu na Kiislamu badala yake yamechagua njia ya kurejesha uhusiano wa kawaida na utawala huo.

Sayed Hassan Nasrallah aliuawa shahidi katika shambulizi kubwa la anga ambalo Israel ilitekeleza kusini mwa Beirut mnamo Septemba 27 kwa kutumia mabomu ya kivita iliyopokea kutoka Marekani.

3490140

Habari zinazohusiana
captcha