Sayed Hassan Nasrallah na Jenerali Niloforoushan, ambaye aliwahi mshauri wa kijeshi nchini Lebanon, waliuawa shahidi katika shambulio la kigaidi la anga la Israel kwenye majengo ya makazi katika kitongoji cha Beirut siku ya Ijumaa.
Baraza la Uratibu wa Maendeleo ya Kiislamu la Iran limesema khitma na hafla ya kuwaenzi mashahidi hao zitaanza saa nane Alasiri Jumatano katika medani ya Imam Hussein (AS) jijini Tehran.
Wananchi waumini wa Tehran wameombwa kushiriki kwa hamasa katika hafla hiyo ambayo pia inafanyika kulaani i jinai za utawala ghasibu wa Israel na kutangaza upya utiifu kwa damu za mashahidi.
Kupitia mahudhurio yao makubwa katika khitma hiyo, wananchi wa Iran watauthibitishia ulimwengu kwamba muqawama au mapambano ya Kiislamu yako hai na njia ya viongozi wake waliouawa shahidi itaendelea milele, ilisema taarifa hiyo.
Baraza hilo pia limesisitiza kuwa, kwa kuwauwa viongozi wa muqawama utawala wa Kizayuni hauwezi kudhoofisha muqawama huo wala hauwezi kugeuza fikra za umma kutokana na kushindwa kwake mbele ya muqawama wa wananchi madhulumu na mashujaa wa Lebanon na Ukanda wa Ghaza.
4239725