IQNA

Muqawama

Ripoti: Namna Marekani ilivyohusika katika mauaji ya Sayyid Hassan Nasrallah

15:33 - October 06, 2024
Habari ID: 3479545
IQNA-Nyaraka na ushahidi uliofichuliwa unaonyesha kuwa ndege mbili za Kimarekani aina ya Boeing E-3 Sentry zenye uwezo wa kusimamia na kudhibiti vita na kutoa picha sahihi za uwanja wa vita, ziliruka katika anga ya Lebanon wakati wa mashambulizi ya utawala wa Kizayuni katika vitongoji vya kusini mwa mji mkuu, Beirut.

Wakati eneo la Hare Harik katika viunga vya kusini mwa mji wa Beirut likikabiliwa na mashambulizi makali ya utawala wa Kizayuni kwa lengo la kumuua Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon Sayyid Hassan Nasrallah, ndege za Marekani zilikuwa zikiruka juu ya ardhi ya Lebanon kwa namna ya ajabu na ya kutia shaka sana.

Taarifa zinasema ndege hiyo ya kijasusi ya jeshi la Marekani ilikuwa ikiruka katika eneo hilo siku ambayo Israel ilimuua kigaidi Sayyid Hassan Nasrallah, na hivyo kuibua swali, je! kuruka kwa ndege aina Boeing E-3 Sentry katika eneo hilo siku hiyo kunaashiria Marekani ilikuwa ikufuatilia mauaji ya Nasrallah?

Ndege hizo mbili aina ya Boeing E-3 Sentry zina vifaa vya usimamizi na udhibiti wa vita, mifumo, ufuatiliaji na utambuzi wa walengwa na uwasilishaji picha za kina za uwanja wa vita.

Rekodi za taarifa na nyaraka za shughuli na rekodi za safari za ndege hizo mbili zinaonyesha kuwa ndege hizi mbili hazijaruka katika maeneo ya Beirut kwa muda mrefu na moja kati yao ilikuwa na safari nje ya visiwa vya Ugiriki mnamo Septemba 19 bila kukaribia ufuo wa Lebanon na hii inaashiria kwamba ndege hizi mbili za Marekani hazikuwa zimepita juu ya eneo la maji ya Lebanon hadi siku ya mauaji ya Sayyid Hassan Nasrallah.

Uchambuzi wa habari na data hizi unaibua maswali juu ya uwepo wa ushirikiano wa kijasusi kati ya Washington na Tel Aviv katika utekelezaji wa shambulio hili la kigaidi dhidi ya harakati ya Hizbullah, ikiwa ni pamoja na iwapo Marekani ilikuwa tayari inafahamu operesheni hii hasa baada ya maafisa wa Marekani kudai kuwa hawakuwa na taarifa.

4239946

Habari zinazohusiana
captcha