IQNA

Muqawama

Wafanyaziara kutoka nchi mbalimbali wahudhuria Arubaini ya Shahidi Nasrallah katika Haram ya Imam Ridha (AS)

15:43 - November 11, 2024
Habari ID: 3479734
IQNA – Idara ya Mfawidhi wa Haram Takatifu ya Imam Ridha (AS) huko Mashhad, kaskazini-mashariki mwa Iran, imeandaa khitma katika eneo hilo takatifu kwa mnasaba wa siku ya Arubaini tokea auawe shahidi  kiongozi wa zamani wa Hizbullah Sayyid Hassan Nasrallah.

Hafla hiyo imehudhuriwa na wafanyaziara kutoka nchi mbalimbali kama vile Lebanon, Iraq, Bahrain, Saudi Arabia, Oman, India na Pakistan.

Katika hotuba yake, mwanachuoni wa seminari na mwakilishi wa Baraza la Dunia la Ahl-ul-Bayt (AS) Hujjatul Islam Alireza Imani Moqaddam alifafanua juu ya ushujaa na tabia ya Nasrallah.

Amesema Katibu Mkuu huyo wa zamani wa Hizbullah alilelewa katika shule ya Imam Hussein (AS) na hakuacha mapambano dhidi ya maadui wa Mwenyezi Mungu hadi dakika za mwisho za uhai wake.

Ameongeza kuwa Shahidi Nasrallah alikuwa mpiganaji asiyechoka katika njia ya Mwenyezi Mungu ambaye aliwapenda Ahl-ul-Bayt (AS) na alitii kikamilifu Wilayat Faqihi.

Hujjatul Islam Imani Moqaddam pia amesisitiza ulazima wa kuchunguzwa vipengele tofauti vya tabia ya shahidi huyo ambaye alikuwa na taathira katika milinganyo ya kieneo na kimataifa na kuligeuza jeshi la utawala wa Israel kuwa chama kilichoshindwa katika vita hivyo.

Mwishoni mwa sherehe hiyo, taarifa ilitolewa ambapo washiriki walitoa heshima kwa Nasrallah na mashahidi wengine wa upinzani wa Kiislamu na kusisitiza utii wao na maadili ya mashahidi.

Sayyid Hassan Nasrallah aliuawa shahidi katika shambulizi kubwa la anga ambalo Israel ilianzisha kusini mwa Beirut mnamo Septemba 27 kwa kutumia mabomu ya kivita yaliyotolewa na Marekani.

Mashambulizi ya Israel yanakuja dhidi ya hali ya mvutano ulioongezeka kati ya vuguvugu la muqawama la Lebanon na kundi linaloikalia kwa mabavu, ambayo ni pamoja na mauaji yaliyolengwa ya makamanda wakuu wa Hizbullah na kulipuliwa kwa vifaa vya mawasiliano vya kundi la muqawama la Waislamu.

Israel imekuwa ikiilenga Lebanon tangu Oktoba 7 mwaka jana, ilipoanzisha vita vya mauaji ya kimbari kwenye Ukanda wa Gaza unaozingirwa.

Hizbullah imekuwa ikijibu uchokozi huo kwa operesheni nyingi za kulipiza kisasi, ikiwa ni pamoja na moja ya kombora la balestiki ya hypersonic, ikilenga ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.

Harakati ya muqawama ya Lebanon imeapa kuendelea na operesheni zake dhidi ya Israel madhali utawala wa Israel unaendelea na vita vyake vya Gaza.

 4247470

Habari zinazohusiana
captcha