IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Iran inashiriki katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Kuwait

21:27 - November 13, 2024
Habari ID: 3479746
IQNA - Iran itakuwa na wawakilishi watatu katika toleo la 13 la mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Kuwait.

Qari na wahifadhi wawili wa Qur'ani wako nchini Kuwait kushiriki katika  Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ambayo yamezinduliwa leo na yantazamiwa kuendellea hadi Novemba 20.
Habib Sedaqat atashindana katika kitengo cha usomaji wa Qur'ani naye Mohammad Reza Zahedi atawania tuzo ya juu katika kitengo cha kuhifadhi Qur'ani Tukufu kwa watu wazima.
Mwakilishi wa Iran katika kuhifadhi Quran nzima kwa ajili ya watoto ni Mohammad Hossein Malekinejad.
Wamechaguliwa kuiwakilisha Iran katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani kwa mujibu wa safu zao katika Mashindano ya Kitaifa ya Qur'ani ya Iran mwaka jana.
Tangu kuanzishwa kwake mwaka wa 2010, mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Kuwait, yanayoandaliwa na Wizara ya Awqaf na Masuala ya Kiislamu ya Kuwait, yanalenga kuwahimiza vijana duniani kote kujihusisha na Qur'ani kwa kuhifadhi na kuisoma.
Mwaka huu; kategoria kadhaa ambazo kuhifadhi Qur'ani nzima, qiraa kwa mitindo kumi ya usomaji,  kuhifadhi kwa vijana, na kategoria maalum ya mradi bora wa kiufundi unaohudumia Qur’ani.
Kuna majaji na washiriki kutoka nchi  85 ambapo miongoni mwa washindani 127, 75 watashiriki katika kategoria ya kuhifadhi, 16 katika kategoria ya mitindo kumi ya qiraa, 13 katika qiraa na 23 katika kategoria ya kuhiadhi kwa vijana.
Maonyesho yenye mada "Kama Ulivyojifunza" yataendeshwa sambamba na shindano hilo. Maonyesho hayo yataonyesha mbinu mbalimbali za kuhifadhi, mitindo ya qiraa ya Qur'ani, na maendeleo katika mbinu za kuhifadhi, na kuwapa waliohudhuria ufahamu wa urithi wa elimu na utamaduni wa Qur'ani.

3490669

captcha