IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Uwezo wa Astan Quds Razavi kutumika kufanikisha Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani  Iran

21:43 - December 31, 2024
Habari ID: 3479979
IQNA – Astan Quds Razavi, Idara ya Mfawidhi wa Haram Takatifu ya Imam Ridha (AS) mjini Mashhad, imeahidi kutoa msaada kamili katika kufanikisha Mashindano ya 41 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu nchini Iran, afisa mmoja amesema.

Hamid Majidimehr, Mkuu wa Kituo cha Masuala ya Qur'ani cha Shirika la Wakfu na Misaada Iran , alitoa kauli hiyo wakati wa mkutano wa pamoja wa maafisa wa Astan Quds Razavi na shirika hilo.

Fainali ya mashindano hayo, ambayo yatafanyika ana kwa ana, itazinduliwa Januari 27, 2025, katika mji mtakatifu wa Mashhad.

Majidimehr amesema kuwa katika toleo hili, Astan Quds Razavi itakuwa chombo kikuu cha kushirikiana na Shirika la Wakfu katika kuandaa mashindano hayo.

Alibainisha kuwa, kwa mujibu wa mipango hiyo, sekta zote za Qur'ani, kitamaduni, usalama, ukaguzi, miundombinu, na matangazo, pamoja na shughuli zozote zinazohusiana na eneo hilo takatifu, zitaendeshwa kwa ushirikiano na Astan Quds Razavi.

Pia alifafanua kuwa katika toleo hili, matangazo ya vyombo vya habari yatafanyika kwa njia maalum, kwa ushirikiano wa pekee kati ya kikundi cha vyombo vya habari cha Astan Quds Ravazi na timu ya vyombo vya habari ya Makao Makuu ya Mashindano ya Quran ya Shirika la Wakfu.

Majidimehr alisema anatarajia maendeleo chanya katika toleo la 41 la mashindano haya.

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huandaliwa kila mwaka na Shirika la Wakfu la Iran.

Lengo la mashindano haya ni kuendeleza utamaduni na maadili ya Qur'ani miongoni mwa Waislamu na kuonyesha vipaji vya wasomaji na wahifadhi wa Qur'ani.

3491274

Habari zinazohusiana
captcha