IQNA

Waislamu wa Tanzania Wajifunza Kuhusu Mafanikio ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran  

17:50 - February 12, 2025
Habari ID: 3480205
IQNA – Semina ya kitamaduni na kielimu iliyopewa jina “Utangulizi wa Mafanikio ya Mapinduzi ya Kiislamu katika Nyanja ya Wanawake” iliandaliwa jijini Dar es Salaam, Tanzania, Jumatatu.

Semina hiyo ilifanyika katika Kituo cha Kiislamu cha Hazrat Masoumah (AS) na iliratibiwa na Kituo cha Kitamaduni cha Iran nchini Tanzania, ikiwa ni maadhimisho ya miaka 46 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

 Mohsen Ma’arefi, Mwambata wa Utamaduni wa Iran nchini Tanzania, alielezea historia ya Mapinduzi ya Kiislamu na kueleza maendeleo na mafanikio ya Iran baada ya ushindi wa mapinduzi, licha ya vikwazo vya kimataifa.

Akitaja maneno ya Imam Khomeini, mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu, alisisitiza kuwa wanawake walikuwa na mchango mkubwa katika ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran aliongeza kuwa: Wanawake walikuwa mbele katika maeneo yote ya mafanikio ya mapinduzi, na hata katika maeneo ambapo wanaume walikuwa mstari wa mbele, wanawake walichukua jukumu muhimu kwa uwepo wao."

Alionyesha filamu inayoonesha mafanikio ya Mapinduzi ya Kiislamu katika nyanja ya wanawake, na kutoa takwimu zinazodhihirisha uwepo mkubwa wa wanawake katika sekta mbalimbali za kijamii, kiuchumi, na kitamaduni baada ya Mapinduzi ya Kiislamu. Alitambulisha pia wanawake kadhaa waliovuna mafanikio makubwa nchini Iran.

Baadaye, washiriki walijiunga na mjadala na kuuliza maswali kuhusu mada mbalimbali, ikiwemo maendeleo yaliyofikiwa nchini Iran katika uwanja wa matibabu ya utasa kwa wanandoa, maendeleo ya chanjo, na mitazamo ya kidini ya Imam Khomeini kuhusu umuhimu wa sayansi za kisasa, ambapo walipata majibu kwa waliyouliza.

Munira Haitham Tajri, mkurugenzi wa Kituo cha Kiislamu cha Hazrat Masoumah (AS), pia alihutubia kikao hicho na alisisitiza umuhimu wa programu hiyo katika kuhamasisha ufahamu miongoni mwa wanafunzi.

Alisema kwamba uzoefu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, hasa katika masuala ya wanawake, ni mfano mzuri kwa wasichana na wanawake wa Tanzania. Kwa kushuhudia uzoefu huu halisi, wanapata kuelewa kuwa fursa za wanawake kushiriki na kuwa na athari katika jamii ni kubwa, aliongeza.

3491823

Habari zinazohusiana
captcha