Semina hiyo ya mtandaoni, iliyopewa jina la “Sayyid Hassan Nasrallah, Fikra ya Kudumu”, iliandaliwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu (WFPIST).
Ilihutubiwa na wanawake wa Kiislamu kutoka Lebanon, Pakistan, Indonesia, Iraq, Yemen, na Syria.
Katika hotuba yake, Raghida al-Misri kutoka Lebanon alisema wanawake wa muqawama wa Lebanon wataendelea kuwa waaminifu katika kumtii Shahidi Nasrallah hata iweje.
"Hata kama nyumba zetu zitaharibiwa, tunasalia katika ardhi yetu na kusimama dhidi ya adui ghasibu," alisema akikusudia utawala haramu wa Israel unaoendeleza mashambulizi ya mauaji ya kimbari dhidi ya Lebanon.
Aliongeza kuwa njia ya Nasrallah na Sira yake itaendelea kufuatwa.
Mzungumzaji mwingine, Fatema Azadimanesh wa Syria amemsifu Shahidi Nasrallah kuwa kiongozi aliyelelewa katika fikra ya Imam Hussein (AS) na kutekeleza mafundisho ya Imam Hussein (AS) katika maisha yake.
Wauda Zeynab Tursani kutoka Indonesia alitoa salamu za rambirambi kwa kuuawa Shahidi Nasrallah na kusema alikuwa mtu mkubwa aliyepigania haki na amani.
Alisema uongozi wake utabakia kuwa kigezo cha kuigwa na vizazi vyote.
Pia aliangazia nafasi ya wanawake katika muendelezo wa njia yake, akisema wanawake ndio nguzo ya muqawama.
Zahra Maldan kutoka Lebanon, ambaye ni mama wa shahidi katika muqawama, alimuelezea Shahidi Nasrallah kuwa ni muumini wa kweli na mfuasi wa njia ya Imam Hussein (AS).
Aliashiria jinsi Shahidi Nasrallah alivyosisitiza umuhimu wa familia na akasema: "Tunapaswa kuwalea watoto wetu kwenye njia ya mafundisho ya Qur'ani Tukufu na shule ya Imam Ali (AS) na Imam Hussein (AS)."
Ameongeza kuwa ili kuendeleza njia ya Sayyid Nasrallah, kujitahidi kuwa na familia yenye kuzingatia maadili na misingi ya elimu ya kidini na Qur'ani ni jambo la maana sana.
Ibtisam al-Shahmani kutoka Iraq alisema ingawa mauaji ya Nasrallah yalikuwa ya uchungu sana, hayatadhoofisha nguvu ya muqawama kwani warithi wake wataendelea na njia yake.
Kwa kauli mbiu ya "Kila siku ni Ashura na kila mahali ni Karbala," Nasrallah alithibitisha kwamba mwamko wa Ashura yanarudiwa kila siku, alibainisha.
“Shahid Nasrallah alitufanya tuwe na Fahari. Aliuawa kishahidi ili kurejesha utu wa mwanadamu. Alitetea ubinadamu wote, "aliongeza.
Wazungumzaji wengine kwenye warsha hiyo ya mtandanoni walifafanua vipengele tofauti vya shakhsia na uongozi wa Shahidi Nasrallah, wakimwita msukumo kwa watu wote wanaokandamizwa duniani.
Sayed Hassan Nasrallah aliuawa shahidi katika shambulizi kubwa la anga la kigaidi lililotekelezwa na utawala katili wa Israel kusini mwa Beirut mnamo Septemba 27 kwa kutumia mabomu ya kivita yaliyotolewa na Marekani.
Israel imekuwa ikiilenga Lebanon tangu Oktoba 7 mwaka jana, ilipoanzisha vita vya mauaji ya halaiki kwenye Ukanda wa Gaza unaozingirwa.
Hizbullah imekuwa ikijibu uchokozi huo kwa operesheni nyingi za kulipiza kisasi, ikiwa ni pamoja na moja makombora , ikilenga ngome za kijeshi na kijasusi za utawala haramu Israel katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala huo.
Harakati ya muqawama ya Hizbullah imeapa kuendelea na operesheni zake dhidi ya Israel madhali utawala wa Israel unaendelea na vita vyake vya mauaji ya kimbari dhidi ya Gaza na Lebanon.
3490286