Wataalamu, watafiti na watu mashuhuri kutoka nchi 30 wanashiriki katika tukio hili la siku mbili, ambalo limefanyika katika Chuo Kikuu cha Shahid Bahonar, kwa mujibu wa Hujjatul Islam Ali Arefi, afisa kutoka kamati ya waandaaji.
Aliyasema haya katika hotuba yake kwenye sherehe za ufunguzi kwamba matembezi ya Arbaeen yamefanyika muda wote wa historia, lakini katika miaka ya hivi karibuni, nyanja zake za kihisia na kidini zimepata umakini zaidi, na kuwa nguvu ya kimataifa.
Arbaeen imeimarisha ustahimilivu kwa sababu inatokana na ushujaa wa Imam Hussein (AS), shujaa na kiongozi wa wanaotafuta uhuru duniani kote, alisema.
Aliongeza kuwa leo, wafuasi wa muqawama wanadhihirisha nguvu zao duniani kote. “Kwa kweli, muqawama umegeuka kuwa alama ya heshima kwenye paji la uso la jamii ya Kiislamu na watafuta uhuru duniani kote. Wafuasi wa Muqawama wanadhihirisha nguvu zao si tu barani Asia bali duniani kote. Uhusiano kati ya Arbaeen na Muqawama ni imara sana, na utamaduni wa Arbaeen kwa kweli umetokana na upinzani. Uhai wa Arbaeen unategemea sana Muqawama huu.”
Kongamano hili linajikita katika mada kama vile Arbaeen na utamaduni wa Muqawama, Arbaeen, sheria na uhusiano wa kimataifa, Arbaeen na uchumi, Arbaeen na roho, maadili na afya, Arbaeen na ustaarabu mpya wa Kiislamu, na Arbaeen na utamaduni wa matarajio.
Arbaeen ni tukio la kidini linalosherehekewa na Waislamu wa Kishia siku arobaini baada ya Siku ya Ashura, ambayo ni sikku ya kukumbuka kuuawa shahidi Imam Hussein (AS), mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW) ambaye pia imam wa tatu wa Kishia.
Ni moja ya mijimuiko mikubwa zaidi ya kidini ya kila mwaka duniani, ambapo mamilioni ya Waislamu wa Kishia hufanya matembezi hadi Karbala kutoka miji mbalimbali ya Iraq na nchi zinazozunguka.
3491831