IQNA

Diplomasia ya Muqawama

Balozi: Wapiganaji wa Yemeni wanakabiliana na Israel kutekeleza wajibu wao wa Qur'ani

20:37 - January 11, 2025
Habari ID: 3480032
IQNA – Msimamo wa Yemen katika mhimili wa muqawama unatokana  na msingi wa Imani, Qur'an Tukufu na mwongozo wa Mwenyezi Mungu, amesema balozi wa nchi hiyo nchini Iran.

Ibrahim Mohammed al-Dailami alitoa kauli hiyo katika mahojiano na Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA), akiongeza kuwa wapiganaji wa Yemeni wameanzisha vita vya kihistoria dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel kwa lengo lakuunga mkono Palestina na kulingana wajibu huu na hawana hofu ya vitisho vya adui.

"Mapambano ya Yemen dhidi ya utawala wa Kizayuni na msaada wake kwa watu wa Gaza si mapambano ya kikundi maalum bali yanakumbatiwa na taifa lote la Yemen. Hii inaonyesha kwamba sehemu mbalimbali za jamii yetu zinashiriki katika mapambano haya kwa njia tofauti. Kwa mfano operesheni za kijeshi za Yemen dhidi ya Israel zinaendeshwa na vikosi vya jeshi la Yemeni na hazijakomea kwa kundi maalum."

Alisema msimamo wa Yemen unatokana na hisia zake za uwajibikaji  kwa mujibu wa Imani kwa mafundisho ya Mwenyezi Mungu katika Qur'ani Tukufu na pia kwa mujibu wa mafundisho ya Mtume Muhammad (SAW). "Hii ni kwa sababu Qur'ani Tukufu ina aya nyingi kuhusu kupambana na makafiri na wanafiki. Zaidi ya hayo, Qur'ani inaonya wale wanaoacha kuunga mkono ukweli kuhusu adhabu ya maumivu."

Amesema Yemen inaweza kuwa mfano kwa Waislamu wengine, hasa mataifa ya Kiarabu, huku akilaani baadhi ya nchi za Kiarabu ambazo zimeegemea upande wa utawala wa Kizayuni na kufumbia macho ukatili wa Israel. Ameendelea kwa kuhoji hivi, 'Iko wapi hisia ya kuwa Mwislamu? Nini kinatokea kwa utekelezaji wa kanuni na maadili ya Qur'ani Tukufu kuhusu wajibu wa kusaidiana kama wanadamu wenzetu? "

Al-Dailami aئثsema kuwa msaada wa taifa la Yemen kwa Palestina hauko tu kwa upande wa kijeshi bali pia kuna maandamano makubwa ya mamilioni nchini humo kwa mshikamano na watu wa Palestina.

"Ingawa wanakabiliwa na magumu ya kiuchumi, watu wa Yemen wamekuwa wakitoa msaada wa kifedha kwa Wapalestina tangu mwanzo wa uvamizi wa Israe na wamekuwa wakikusanya michango kwa taifa la Palestina. Kwa hiyo, changamoto hizi za kiuchumi hazikuwazuii kufanya Jihad (mapambano katika njia ya Mungu) kwa mali zao na maisha yao."

Pia ameisitiza msaada wa watu wa Yemen kwa Palestina katika mitandao ya kijamii pamoja na kususia bidhaa za Israeli na zile zinazozalishwa na wafuasi wa utawala wa Kizayuni.

Ameeleza zaidi kuwa msingi wa harakati za watu wa Yemen ni uhusiano wao na Qur'ani Tukufu, na fadhila hii, baada ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, inahusishwa na shahidi Sayed Hussein Badreddin al-Houthi.

"Alianza mradi wake wa Qur'ani Tukufu mnamo 2001, ambao unajumuisha hotuba na masomo yanayoshughulikia masuala muhimu kuhusu mwongozo na baraka za Qur'ani Tukufu. Ninawaalika watu wote wenye heshima, watafiti, na kila mtu katika jamii ya Kiislamu kurejea kwenye masomo haya ya Qur'ani na kupata uelewa wa asili ya mradi wa Qur'ani uliowasilishwa na Sayed Hussein Badreddin al-Houthi.

"Ametoa wito wa kuzingatia kudumisha mwongozo wa Qur'ani katika kuongoza watu. Quran Tukufu sio tu kwa ibada na usomaji. Ni kitabu cha mwongozo kutoka kwa Mwenyezi Mungu kinachoelezea njia ya heshima na heshima kwa sisi katika dunia hii na akhera. Qur'ani Tukufu ni kamba ya Mungu, inayotoka mbinguni hadi duniani, lakini kwa bahati mbaya, Waislamu wengi wameweka kando Qur'ani na badala yake wanageukia nadharia, mawazo, na madhehebu ambayo yanawazungusha mbali sana na Qur'ani na umuhimu wake."

/3491407

Habari zinazohusiana
captcha