IQNA

Muqawama (Mapambano ya Kiislamu)

Hizbullah: Hatuogopi vitisho vya Israel, tunaamini kuwa tutashinda

20:29 - November 17, 2023
Habari ID: 3477901
BEIRUT (IQNA)- Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon ameongeza kuwa, "Kuhusu kuenea kwa vita, uwezekano huo upo, iwapo watatushambulia, tutalazimika kujihami na tutatumia nguvu zetu zote. Hatuogopi vitisho vya Israel, tunaamini kuwa tutashinda."

Sheikh Naim Qassim amesema hayo katika mahojiano na gazeti la El Mundo la Uhspania na kueleza kuwa, kuna haja ya kushambulia milki za Marekani kwa shabaha ya kusimamisha uvamizi na mashambulizi ya kinyama ya Israel dhidi ya wakazi wa Gaza.

Sheikh Naim Qassim amesema, Hizbullah hivi sasa ipo katika hali bora zaidi ikilinganishwa na mwaka 2006 ilipopigana na Israel kwa siku 33, na kwamba harakati hiyo ya muqawama hivi sasa inamiliki mabohari yaliyojaa silaha.

Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema utawala haramu wa Israel utasambaratishwa na kufutwa katika uso wa dunia iwapo utajaribu kuwafurusha wananchi wa Palestina wanaoshi katika Ukanda wa Gaza.

Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema utawala haramu wa Israel utasambaratishwa na kufutwa katika uso wa dunia iwapo utajaribu kuwafurusha wananchi wa Palestina wanaoshi katika Ukanda wa Gaza.

Sheikh Qassim amebainisha kuwa, "Iwapo Israel itaamua kuendeleza uvamizi wake, itakuwa inajichimbia kaburi lake na kutoa fursa mwafaka ya kuangamizwa kimalifu."

Amesema Hizbullah imejaribu kuuzuia utawala huo pandikizi usiendeleza mashambulizi dhidi ya raia katika Ukanda wa Gaza, na kusisitiza kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kutanuka na kuenea vita hivyo iwapo Israel haitasitisha hujuma zake. 

Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kislamu ya Hizbullah ya Lebanon  amesisitiza kuwa, hakuna shaka njama na mipango yote ya utawala dhalimu wa Israel itashindwa na kugonga mwamba.

Kiongozi huyo wa kidini wa Lebanon ameeleza bayana kuwa, "Idadi ya raia wa Kipalestina wanaouawa shahidi na Israel inaongezeka siku baada ya siku, tuna mpango wa kujibu mashambulizi haya na kuilazimisha Israel isalimu amri. Huu ni uamuzi ambao tutautekeleza katika medani ya vita."

 

 4182227

Habari zinazohusiana
captcha