IQNA

Hija

Teksi za kuruka, ndege zisizo na rubani kutumika kwa majaribi katika Hija

10:52 - May 12, 2024
Habari ID: 3478804
IQNA- Matumizi ya teksi zinazoruka na ndege zisizo na rubani kwa ajili ya kuwasafirisha Mahujaji yatafanyiwa majaribio katika msimu wa Hija wa mwaka huu.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Uchukuzi na Usafirishaji wa Saudi Arabia, Saleh Al-Jasser.

"Kuna mashindano kati ya makampuni mengi maalum katika sekta ya usafiri ili kutoa njia bora ya usafiri katika miaka ijayo," Al-Jasser alisema.

Kwa mujibu taarifa, waziri huyo alisema Saudi Arabia inatayarisha teknolojia na vyombo vya usafiri vinavyobadilika na kasi zaidi katika msimu wa Hija wa mwaka huu ili kurahisisha safari ya hujaji.

"Kwa hiyo, ni lazima tuwe mstari wa mbele ili kufaidika na huduma hizi," aliongeza. Mapema mwaka huu, Shirika la Ndege la Saudi Arabia pia lilifichua mipango ya kuendesha teksi zinazoruka kuwasafirisha mahujaji kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mfalme wa Abdulaziz mjini Jeddah hadi hoteli za Makka. Saudi Arabia inakusudia kununua takriban ndege 100 ili kuendesha huduma hiyo.

Hija, moja ya nguzo za Uislamu, ni hija ya kila mwaka ya mji mtakatifu wa Makka. Msimu wa Hajj wa mwaka huu unatarajiwa kuanza Katikati ya Juni.

3488280

Habari zinazohusiana
Kishikizo: hija
captcha