IQNA

Ubunifu katika usomaji wa Maqariwa Iran: Mada Kuu ya Mkutano wa 20 wa Wataalamu wa Qur’ani

20:58 - July 21, 2025
Habari ID: 3480976
IQNA – Mkutano wa 20 wa wataalamu wa Qur’ani, makari na wahifadhi wa Iran utafanyika mwezi Novemba mwaka huu chini ya usimamizi wa Baraza Kuu la Qur’ani.

Mkutano huo utazingatia mada ya “Mahitaji ya Ubunifu katika Usomaji wa Maqari wa Iran”, ikiwa ni juhudi za kuendeleza sanaa ya usomaji wa Qur’ani kwa njia za kisasa na zenye mvuto wa kiroho.

Kwa mujibu wa Idara ya Mawasiliano ya Baraza Kuu la Qur’ani, mikutano hii maalum ya wataalamu mashuhuri wa Qur’ani ni miongoni mwa matukio makubwa ya Qur’ani nchini Iran. Toleo la mwaka huu litakuwa la 20, likiwa ni ishara ya kuingia katika muongo wa pili wa shughuli hizi za kitaalamu.

Mohammad Taqi Mirzajani, Mkuu wa Elimu, Utafiti na Mawasiliano wa Baraza hilo, alisema kuwa mikutano ya awali imejadili mada mbalimbali zinazohusiana na jamii ya wasomaji wa Qur’ani nchini humo.

Aliongeza kuwa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu alionesha kuridhika na mada zilizojadiliwa katika mikutano hiyo, jambo linaloashiria mafanikio ya harakati hii ya kielimu na kitaalamu ya Qur’ani.

Mirzajani alifafanua kuwa mwanzoni mwa mwezi wa Ramadhani uliopita, kiongozi huyo alitoa maono ya juu kwa wataalamu na wasomaji wa Qur’ani nchini Iran, akihimiza ubunifu wa lahani mpya katika usomaji wa Qur’ani, kwa kuzingatia maendeleo ya kitaaluma yaliyopatikana kwa miaka mingi.

Kwa msingi huo, mkutano wa 20 utaangazia mahitaji ya ubunifu katika usomaji wa maqari wa Iran, ikiwa ni pamoja na tabia, muonekano wa wasomaji wa Qur’ani, na ushiriki wao katika shughuli za kijamii.

 Mkutano huo utafanyika mwezi Novemba, na wataalamu wa Qur’ani wanakaribishwa kuwasilisha makala, mipango na mawazo yao kuhusu mada zilizoteuliwa kabla ya katikati ya Oktoba.

3493927

Kishikizo: iran qurani tukufu
captcha