Talal Atrisi alitoa kauli hiyo katika mkutano wa mtandaoni ulioandaliwa na IQNA kwa jina “Heshima na Nguvu ya Iran; Ujumbe Ulio Zaidi ya Makombora”, uliofanyika Jumamosi. Washiriki wengine walikuwa Danial Bin Mohammad Yusof kutoka Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Kimataifa Malaysia, Dina Sulaeman kutoka Indonesia, na mchambuzi wa Kipalestina Iyad Abu Nasser.
Mkutano huo ulifanyika kufuatia mashambulizi ya siku 12 ya Marekani na Israel dhidi ya Iran, yaliyoanza Juni 13. Baada ya mashambulizi hayo ya kichokozi Iran ilijibu kishujaa na kuwaadhibu wavamizi. Katika hotuba yake, Atrisi alieleza kuwa operesheni ya Ahadi ya Kweli 3 iliyotekelezwa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilikuwa jibu la kujihami dhidi ya uchokozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel na Marekani Alifafanua kuwa mashambulizi hayo yalifanyika kwa misingi miwili:
1. Muktadha wa kwanza: Wakuu wa utawala wa Kizayuni walitangaza mara kadhaa nia ya kuunda “Mashariki ya Kati Mpya”. Kuanguka kwa serikali ya Syria, kuingilia kwa Israel nchini humo, na kutawala maeneo mbalimbali ya Syria kulimfanya adui Mzayuni aamini kuwa nchi zote za Mashariki ya Kati zingeweza kutawaliwa kutoka Tel Avivi , huku Iran ikiwa kizuizi kikuu.
2. Muktadha wa pili: Mazungumzo kati ya Iran na Marekani kuhusu mustakabali wa mpango wa nyuklia wa amani wa Iran.
Mashambulizi ya Marekani na Israel Yavuruga Mazungumzo ya Amani; Iran Yazima Mpango wa “Mashariki ya Kati Mpya”
Mashambulizi hayo yalivuruga mchakato wa mazungumzo ya amani, na kutumbukiza eneo la Mashariki ya Kati au Asia Magharibi katika hali ya taharuki, hofu na wasiwasi. Vita vikali na vya kuumiza vilizuka kati ya pande hizo mbili.
Kwa mujibu wa matamshi, taarifa na msimamo wa taasisi mbalimbali za Israel, Marekani, na vyombo vya habari, lengo halisi la adui halikuwa tu mpango wa nyuklia wa Iran. Mauaji ya makamanda, idadi ya mamluki waliokuwa wakifadhiliwa na utawala wa Kizayuni kwa miaka mingi, havikuwa na uhusiano wowote na nyuklia.
Lengo lao lilikuwa ama kuangusha mfumo wa Iran au kuleta machafuko ya ndani. Kama mpango huo ungefanikiwa, utawala wa Kizayuni ungepata fursa ya kutekeleza mpango wake wa “Mashariki ya Kati Mpya”, kwa sababu Iran ingekuwa dhaifu, imegawanyika, na isiyo na usalama au, katika hali ya udhaifu, Iran ingeingia kwenye mazungumzo na Marekani.
Hii ndiyo maana ya kauli yao kuwa Iran inapaswa “kujisalimisha kikamilifu”. Wanachotaka ni kuiondoa Iran kama taifa imara lenye uwezo wa kushughulikia masuala ya kikanda, hasa suala la Palestina, na lenye uwezo wa nyuklia na makombora. Kuangamiza uwezo huo kungefungua njia ya “Mashariki ya Kati Mpya” isiyo na upinzani dhidi ya mradi wa Marekani na Israel.
Lakini kilichotokea na kilicho na umuhimu mkubwa wa kimkakati ni kwamba Iran ilizima mpango huo. Ingawa ilikumbwa na usaliti wa kidiplomasia na ilipata hasara, iligundua njama za ndani na usaliti wa watu katika maeneo mbalimbali na iliweza kujikusanya upya ndani ya saa chache. Huo ndio ulikuwa wakati ambapo mradi wa Marekani na Israel ulifeli.
Iran iliporejea nguvu zake, ilishambulia kwa nguvu taasisi za kijeshi, kiuchumi na kiusalama za utawala wa Kizayuni wa Israel, na kuibua mafanikio ya kihistoria yasiyokuwa na mfano.
Ni kweli kwamba Iran ilipoteza makamanda wake wa kihistoria na kulipa gharama kubwa, lakini kwa mara ya kwanza katika historia ya utawala wa Kizayuni wa Israel, anga zake, ambazo zilidaiwa kuwa haziwezi kukiukwa, zilisambaratishwa na Iran, na mji mkuu Tel Aviv—uliokuwa ukionekana kuwa salama dhidi ya kombora lolote uliharibiwa.
Iran imefanikiwa kuzuia mpango wa Marekani na Israel wa kuunda “Mashariki ya Kati Mpya”, na sasa Waziri Mkuu wa Israel, Netanyahu, haizungumzi tena kuhusu mpango huo. Badala yake, ameanza kuzungumzia mazungumzo mapya na Syria ili kurejea kwenye Mkataba wa Abraham na sera za kawaida za mahusiano zilizokuwepo kabla ya Operesheni ya Mafuriko ya Al-Aqsa.
Hili ni tukio muhimu, mpango huo umeshindwa na kusitishwa. Aidha, kiwango cha utegemezi wa Israel kwa Marekani kimefichuliwa. Bila msaada wa Marekani, Israel isingeweza kuendeleza vita hiyo kwa zaidi ya siku chache. Ililazimika kuomba msaada wa Rais wa Marekani ili kushambulia vituo vya nyuklia vya Iran, ambavyo kwa mujibu wa ripoti, viliharibiwa kidogo tu na vinaweza kurejea kazini ndani ya miezi michache.
Hatua ya Iran ilikuwa pigo kali kwa mradi wa Israel, lakini jambo jingine muhimu ni kwamba Iran ilijibu uchokozi wa Marekani katika Ghuba ya Uajemi huku ikidumisha mahusiano chanya na nchi jirani—ikiwemo Qatar ambako kituo cha Marekani kilishambuliwa kwa mafanikio kwa makombora ya Iran. Hii inaonyesha kuwa Iran ina nia ya kuimarisha mahusiano ya ujirani mwema hata wakati wa mzozo.
Katika siku zijazo, Iran inaweza kutumia nafasi hii, baada ya kuthibitisha kuwa ni taifa lenye nguvu na ujasiri, kuhamasisha nchi za Ghuba ya Uajemi kuangalia upya mahusiano yao na Iran kwa mtazamo chanya. Ushirikiano wa nchi hizo na Marekani au Israel dhidi ya Iran unaweza kufifia, na badala yake kugeuka kuwa ushirikiano wa kiusalama na kisiasa na Iran.
Mkutano kati ya Waziri wa Ulinzi wa Saudi Arabia na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, ni sehemu ya mwelekeo huu. Vilevile, kuboreka kwa mahusiano kati ya Misri na Iran kunaonyesha kuwa nchi za kikanda sasa zinaiona Iran kama nguvu kuu inayoweza kukabiliana na madola ya kimataifa, na hivyo kushirikiana nayo ni bora kuliko kujiunga na wengine. Israel, licha ya kuwa na mahusiano ya kawaida na baadhi ya nchi, bado haionekani kuwa mshirika wa kuaminika.
Kwa upande wa Iran, mabadiliko haya yameiwezesha kugundua njama za ndani, kujaribu uwezo wake, na kuanza kuujenga upya kwa msingi wa mafunzo yaliyopatikana kutokana na vita hii.
Katika ngazi ya kikanda, bado hatuwezi kusema kuwa Asia ya Magharibi iko katika hali ya amani, kwani uwezekano wa vita bado upo. Faili la vita kati ya Iran na utawala wa Kizayuni bado halijafungwa. Syria, nchi ya kiungo katika Asia ya Magharibi, bado haijapata amani. Kwa hivyo, eneo hilo halitakuwa tulivu kikamilifu katika siku zijazo. Muungano mpya utaibuka, na kama ilivyosemwa, nchi za Ghuba ya Uajemi zitazidi kuelekea kushirikiana na Iran kutokana na hofu ya upanuzi wa Israel nchini Syria.
Licha ya matukio haya yote na uwezekano wa vita mpya au uchokozi wa Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mwaka mmoja, miwili au mitatu ijayo, ninaamini kuwa hali ya ndani ya Iran imeimarika zaidi, mfumo wake umeungana kwa uthabiti, na wananchi wake wamezidi kuungana na serikali yao.
Nchi za kikanda sasa ziko tayari zaidi kushirikiana na Iran, huku Marekani ikizidi kujitenga na rais wake kuonekana kutokuwa wa kuaminika kutokana na ahadi zilizovunjwa—akizungumza kuhusu diplomasia lakini akitekeleza uchokozi.
Sera ya Israel ya kupanua maeneo inayoyakalia kwa mabavu haikubaliki na yeyote. Kwa hivyo, tunakabiliwa na mabadiliko makubwa ya kisiasa katika eneo hili. Ingawa uchokozi dhidi ya Iran ulikuwa na gharama kubwa, pia ulikuwa fursa ya Iran kupanua uwezo wake na mahusiano yake, na kufungua njia ya Mashariki ya Kati mpya ya Kiirani-Kiarabu-Kiisilamu ambako Israel imeondolewa, na eneo hili halitakuwa tena kama Israel ilivyotaka kulibadilisha.
Insha’Allah, tutaendelea mbele katika njia hii.
3493906