IQNA

Mapambano dhidi ya Israel

Makombora ya cruise ya Yemeni yalenga vituo vya kijeshi vya Israel

13:05 - November 23, 2023
Habari ID: 3477933
SANAA (IQNA) - Yemen imevurumisha makombora ya cruise dhidi ya maeneo ya kijeshi ya utawala wa Kizayuni wa Israel

Vikosi vya Wanajeshi vya Yemen siku ya Jumatano vilitangaza kuanzisha mashambulizi mengine dhidi ya maeneo yanayokaliwa kwa mabavu ili kuwaunga mkono Wapalestina katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, ambao wanateseka kutokana na uvamizi usiokoma wa Israel.

Sambamba na kuendelea mashambulizi ya mabomu ya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza kwa kipindi cha mwezi mmoja na nusu uliopita, uwezekano wa kupanuliwa maeneo ya vita daima limekuwa jinamizi baya zaidi kuwahi kufikiriwa na Wazayuni katika vita hivyo.

Jinamizi hilo limekuwa likidhihiri taratibu tangua kuanza mashambulio ya kinyama ya mabomu ya utawala huo ghasibu huko Gaza ambapo Hizbullah ya Lebanon imekuwa ikishambulia maeneo ya Wazayuni kusini mwa nchi hiyo, na hivi sasa, katika siku za karibuni, vikosi vya muqawama vya Yemen vimefungua mstari mpya wa vita dhidi ya watendajinai wa Kizayuni huko katika Bahari Nyekundu au kwa jina jingine Bahari ya Sham. Hatua ya karibuni ya kushtukiza ya vikosi vya Yemen dhidi ya utawala wa Kizayuni ilitimia kupitia kukamatwa meli ya mfanyabiashara wa Kizayuni siku ya Jumapili.

Katika taarifa yake kuhusu kutekwa meli hiyo ya utawala wa Kizayuni katika Bahari ya Sham, jeshi la Yemen limesisitiza kuwa meli zote za utawala huo pamoja na nyingine zinazoshirikiana na utawala wa kibaguzi wa Tel Aviv sasa zitakuwa shabaha halali ya jeshi la Yemen.

Brigedia Jenerali Yahya Saree, Msemaji Rasmi wa Vikosi vya Wanajeshi wa Yemen amesema: Jeshi la Wanamaji la Yemen linakwenda sambamba na utekelezaji wa amri ya Kiongozi Mkuu (Abdul Malik Badr al-Din al-Houthi) na katika kujibu matakwa ya taifa kubwa la Yemen na watu wote walio huru katika Umma na kwa kuzingatia majukumu ya kidini, kibinadamu na kimaadili kwa taifa la Palestina, limeendesha operesheni ya kijeshi katika Bahari ya Sham, ambapo limekamata meli ya Israel na kuipeleka katika pwani ya Yemen.

Mohammed al-Bakhiti, mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya Ansarullah ya Yemen pia amesema katika mazungumzo na televisheni ya Al-Jazeera kwamba ikiwa vita dhidi ya Gaza havitasimama, tutakuwa na machaguo mengi mbele yetu.

Zaifullah al-Shami, Waziri wa Habari wa Serikali ya Wokovu wa Kitaifa ya Yemen amesema kuhusu kutekwa meli hiyo ya Kizayuni katika Bahari ya Sham na wapiganaji wa Yemen kwamba: 'Tuna taarifa kamili kuhusu meli zote za Israel zinazopita katika Bahari ya Sham.'

Ali al-Kahhoum, mjumbe wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Ansarullah ya Yemen ametangaza kuwa, nchi yake inaendelea na operesheni za kuvuka mpaka ili kuiunga mkono Gaza na Palestina.

Muhammad Abdus Salaam, Msemaji wa Ansarullah ya Yemen amebainisha kuwa, juhudi zozote za kuzuia kuenea wigo wa mizozo zinategemea kusitishwa uvamizi wa utawala ghasibu wa Israel na kusisitiza kuwa, operesheni ya kukamatwa kwa meli hiyo ya Israel ni mwanzo tu wa mambo na ulimwengu unapasa kujua kwamba jinai za utawala ghasibu wa Israel huko Gaza zimekiuka mipaka na sheria zote za kimataifa.

3486135

 

Kishikizo: yemen gaza palestina israel
captcha