
Hii inapingana na mtazamo wa zama za Jahiliyyah (kabla ya Uislamu), ambapo watu walikuwa wakisema: “Msaidie nduguyo awe mwenye kudhulumu au kudhulumiwa.” Mtazamo huu umeingia pia katika siasa za kisasa, ambapo mataifa huungana bila kujali haki au dhulma na hivyo kusaidiana hata pale mmoja anapokuwa mnyanyasaji.
Ikiwa jamii za Kiislamu zitashirikiana katika mambo ya kujenga, bila kuangalia upande wa kisiasa au ukoo, na wakaacha kusaidia madhalimu, basi matatizo mengi ya kijamii yataisha. Vivyo hivyo, ikiwa mataifa duniani yataacha kushirikiana na wavamizi, basi dhulma na uonevu vitatoweka.
Mtume Muhammad (SAW) amesema: Siku ya Kiyama, mwenye kunadi atauliza: Wako wapi madhalimu na washirika wao? Wale waliowasaidia kwa kalamu, mikoba, au hata wino; nao wakusanywe pamoja na madhalimu.
Qur’ani Tukufu pia inasema (Surah At-Tawbah, aya ya 24): Sema: Ikiwa baba zenu, na wenenu, na ndugu zenu, na wake zenu, na jamaa zenu, na mali mliyo yachuma, na biashara mnazo ogopa kuharibika, na majumba mnayo yapenda, ni vipenzi zaidi kwenu kuliko Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Jihadi katika Njia yake, basi ngojeni mpaka Mwenyezi Mungu alete amri yake. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wapotovu.
Hii inaonyesha kuwa mapenzi ya familia na mali ni halali, lakini hayapaswi kushinda mapenzi kwa Allah na Mtume Wake. Ikiwa mapenzi ya kidunia yatashinda dini, basi mtu huingia katika maasi na hupoteza uongofu.
3495102