
Ukuta mmoja na angalau nakala tatu za Qur’ani Tukufu pamoja na mazulia ya msikiti huo vilichomwa moto, kama ilivyoshuhudiwa na mwandishi wa shirika la AP siku ya Alhamisi.
Upande mmoja wa msikiti ulipakwa maandiko ya grafiti yenye ujumbe wa vitisho kama vile: “hatuna hofu,” “tutalipiza tena,” na “endeleni kulaani.”
Hii ni mfululizo wa mashambulio ambayo yamezua wasiwasi kutoka kwa maafisa wakuu, viongozi wa kijeshi na pia serikali ya Marekani.
Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni walikuwepo eneo la tukio, ingawa hawakutoa maelezo mara moja.
Kwa mujibu wa ripoti, vijana wavamizi wamefanya mamia ya mashambulio tangu Israel ilipoanzisha vita vya kikatili dhidi ya Gaza miaka miwili iliyopita. Mashambulio haya yameongezeka katika wiki za hivi karibuni wakati Wapalestina wakivuna miti yao ya mizeituni, ibada ya kila mwaka. Oktoba imekuwa mwezi wenye idadi kubwa zaidi ya mashambulio ya wavamizi Ukingo wa Magharibi tangu Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Misaada ya Kibinadamu ianze kurekodi takwimu mwaka 2006.
Jumanne iliyopita, makumi ya wavamizi wa Kiyahudi wakiwa wamevaa barakoa walishambulia vijiji vya Beit Lid na Deir Sharaf, wakichoma magari na mali nyingine kabla ya kukabiliana na wanajeshi wa Kizayuni.
Wapalestina na wanaharakati wa haki za binadamu wanailaumu jeshi na polisi la Israel kwa kushindwa kukomesha mashambulio ya wavamizi.
3495388/