IQNA

Waislamu Uingereza

Mashirika ya Kiislamu ya Uingereza yaitaka serikali izuie chuki dhidi ya Uislamu

22:44 - August 30, 2024
Habari ID: 3479352
IQNA - Takriban mashirika 80 ya Kiislamu na viongozi wa jamii za Waislamu wametoa wito kwa serikali ya Uingereza kuchukua hatua madhubuti ili kukabiliana na ongezeko la chuki dhidi ya Uislamu nchini humo.

Katika taarifa yake, mashirika na viongozi walioungana chini ya muungano wa kupambana na chuki dhidi ya Uislamu, wameangazia kuwa jambo la kawaida chuki dhidi ya Uislamu, jambao ambalo  hivi karibuni limesababisha ghasia katika miji kadhaa.

Waliitaka serikali kupitisha rasmi ufafanuzi wa Kundi la Wabunge wa Vyama Vyote (AAPG) wa chuki dhidi ya Uislamu au Islamophobia "ili kutuma ujumbe wazi kwamba hakutakuwa na uvumilivu kwa wenye chuki dhidi ya Uislamu."

Taarifa hiyo pia ilitaka uchunguzi huru kuhusu jukumu la majukwaa ya mitandao ya kijamii, vyombo vya habari vya kawaida, na mitazamo ya yenye  kueneza chuki na chuki dhidi ya Uislamu.

"Serikali lazima ishirikiane moja kwa moja na wawakilishi halali, waliochaguliwa kidemokrasia wa jumuiya za Kiislamu, hasa Baraza la Waislamu la Uingereza, ili kuhakikisha kwamba sauti za Waislamu zinasikika na kushughulikiwa," iliongeza taarifa hiyo.

Kauli hiyo ilitolewa huku kukiwa na msukosuko wa hivi majuzi nchini Uingereza, ambapo waasi wa mrengo mkali wa kulia waliwalenga Waislamu, makundi ya walio wachache na wahamiaji kwa matamshi ya ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya Uislamu.

Ghasia hizo zilichochewa na madai ya uwongo mtandaoni kwamba mshukiwa aliyekamatwa kwa mauaji ya watoto watatu Julai 29 huko Southport alikuwa mwislamu mtafuta hifadhi.

Mamlaka imemtambua mshambuliaji huyo kama Axel Rudakubana, mwenye umri wa miaka 17 aliyezaliwa Cardiff na wazazi wa Rwanda na hakuwa Mwislamu, lakini Pamoja na hayo chuku dhidi ya Uislamu zinaendelea nchini humo.

3489702

Habari zinazohusiana
captcha