
Mohamed al-Maamoun al-Qasimi al-Hosni amesema shughuli za msikiti kwa sasa zimejikita katika kushirikiana na vituo vya kielimu vya Kiarabu, Kiislamu na Kiafrika ili kuimarisha nafasi ya msikiti huu katika uwanja wa kielimu na kidini duniani.
Ameongeza kuwa Dar-ul-Qur'an inajiandaa kupokea kundi la kwanza la wanafunzi wa kimataifa wa PhD. Msikiti Mkuu wa Algiers umejizatiti kutekeleza jukumu pana la kimaendeleo ya ustaarabu, na kwa mujibu wa maono yaliyotangazwa na Rais Abdelmadjid Tebboune wakati wa uzinduzi wa jengo hili kubwa la kidini, msikiti utakuwa ngome ya mamlaka ya kidini. Al-Qasimi alibainisha kuwa tayari mafanikio mengi yamepatikana kupitia taasisi na mashirika yanayohusiana na Msikiti Mkuu wa Algiers, na miradi hiyo inaendelezwa sambamba na jukumu la kitamaduni ambalo msikiti unalenga kulitekeleza.
Ni vyema kutambua kuwa Dar-ul-Qur'an ni moja ya idara za Msikiti Mkuu wa Algiers na mojawapo ya mashirika yaliyojumuishwa ndani ya msikiti huu, ambayo yameweka elimu ya kidini na isiyo ya kidini katika ajenda yake.
Dar-ul-Qur'an ni chuo cha elimu ya juu katika nyanja za sayansi za Kiislamu na kidini, na inalenga kufundisha wanafunzi mahiri katika ngazi ya uzamivu kwa mihula minne ya kitaaluma. Wanafunzi wa PhD wanatakiwa kukamilisha kozi ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu.
Miongoni mwa masomo yanayofundishwa katika Dar-ul-Quran ni Qur'ani Tukufu na Elimu ya Kidini, Qur'ani Tukufu na Mazungumzo kati ya Tamaduni na Utamaduni, Qur'ani Tukufu na Imani na Sayansi ya Tabia, Bima ya Takaful (mfumo wa bima ya Kiislamu), FinTech (Teknolojia ya Fedha), Masoko ya Fedha za Kiislamu, Historia ya Sayansi na Hisabati, Saikolojia ya Kijamii kwa mtazamo wa Uislamu, Saikolojia ya Elimu, Saikolojia ya Elimu kwa mtazamo wa Uislamu, Urithi wa Kijengo, na Mipango na Maendeleo ya Miji.
3495557