IQNA

Mashindano ya Kitaifa ya Usomaji Qur’ani Yazinduliwa Algeria

20:05 - December 02, 2025
Habari ID: 3481604
IQNA – Toleo la 21 la mashindano ya kitaifa ya Qur’ani Tukufu nchini Algeria limeanza rasmi Jumatatu.

Waziri wa Awqaf na Mambo ya Kidini, Youcef Belmehdi, alizindua duru za mchujo za kitaifa za Tuzo ya Algiers ya Usomaji wa Qur’ani katika mji mkuu, Algiers, jana.

Mashindano haya, yanayofanyika chini ya udhamini wa Rais wa nchi hiyo, Abdelmadjid Tebboune, yamekusanya takribani washiriki 120 kwa awamu ya mchujo, iliyoanzishwa na Belmehdi katika makao makuu ya wizara, kwa mujibu wa taarifa ya wizara.

Mashindano yamegawanywa katika makundi matatu, huku duru za mchujo zikifanyika kwa siku tatu kupitia videoconference, chini ya usimamizi wa jopo maalum la wataalamu wa kanuni za usomaji wa Qur’ani.

Algeria ni nchi ya Kiarabu iliyoko Afrika Kaskazini, ambapo Waislamu wanakadiriwa kuwa asilimia tisini na tisa ya idadi ya watu wake.

3495596

Kishikizo: algeria qurani tukufu
captcha