
Akizungumza na IQNA, Hujjatul‑Islam Mohammad Ali Ayazi alisema kuwa vitendo hivyo ni uhalifu wa kivita na vinaonyesha tabia isiyokubalika ya wavamizi.
Aidha aliikosoa jamii ya kimataifa kwa kubaki kimya mbele ya vitendo hivyo.
Hujjatul‑Islam Ayazi pia alilaani zaidi kutochukua hatua kwa taasisi kama UNESCO, na akatoa wito kwa wasomi huru wa seminari na vyuo vikuu kuvunja ukimya na kulalamika waziwazi katika majukwaa ya kimataifa.
“Kulingana na sheria zote za kimataifa, vitendo kama hivi bila shaka vinachukuliwa kuwa uhalifu wa kivita na vinakataliwa kikamilifu na jumuiya za kimataifa,” alisisitiza.
Ameongeza kuwa maadui hushambulia hata madaraja ya mijini bila sababu yoyote, ilhali ni mali ya wananchi, lakini wavamizi wanatafuta visingizio vya kuhalalisha matendo yao yasiyo sahihi.
Alieleza kuwa vitendo hivyo si chochote ila ni unyanyasaji na uadui wa kiwango cha juu dhidi ya taifa la Iran, na ni kinyume kabisa na sheria.
Kuhusu kukosekana kwa mwitikio ufaao kutoka kwa baadhi ya taasisi za kimataifa, hasa UNESCO, Hujjatul‑Islam Ayazi alisema: “Taasisi za aina hii huwa na sababu wanazojitetea nazo; ikiwa ni pamoja na ukweli kwamba sehemu ya ufadhili wao hutoka kwa baadhi ya madola, ikiwemo Marekani, na hivyo huwa waangalifu ili misaada hiyo isikatwe.”
Kuhusu nafasi ya wasomi wa Hawzah na vyuo vikuu, alisema kuwa wasomi hao wanapaswa kulaani mashambulizi dhidi ya vituo vya kisayansi na kitamaduni, na kufikisha malalamiko yao kwa taasisi za kimataifa za kielimu na kitamaduni kupitia barua na kauli rasmi.
3497071