IQNA

Wahifadhi 333 wa Qur’ani Waenziwa Istanbul

17:05 - April 27, 2026
Habari ID: 3482168
IQNA – Hafla maalumu imefanyika katika mji wa Istanbul, Uturuki, kwa ajili ya kuwatunuku zaidi ya wahifadhi 300 wa Qur’ani Tukufu.

Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdoğan, alihudhuria hafla hiyo ya kuhitimu kwa kundi la wahifadhi hao. Hafla hiyo ilifanyika Ijumaa iliyopita, tarehe 24 Aprili 2026, kabla ya Swala ya Ijumaa.

Jumla ya wanafunzi 333 wa hifdh ya Qur’ani, waliopata mafunzo katika shule za maimamu na wahubiri pamoja na taasisi za kuhifadhisha Qur’ani, walihitimu katika hafla hiyo.

Wahifadhi hao walihudhuria hafla wakiwa wamevalia mavazi yaliyopambwa kwa bendera za Uturuki na Palestina, ishara ya mshikamano wa Kiislamu.

Baada ya hafla hiyo, Rais Erdoğan alishiriki Swala ya Ijumaa katika eneo hilo hilo pamoja na ujumbe wake.

Khutba ya Ijumaa ilitolewa kwa lugha ya Kituruki, na pia kwa Kiarabu, Kiingereza na Kijapani, katika kuakisi wigo mpana wa ujumbe wa Kiislamu kwa walimwengu.

3497240

captcha