
Ayatullah Khamenei amebainisha haya katika ujumbe wake leo Alhamisi kwa mnasaba wa kukumbuka kutimia mwaka wa 37 tangu kuaga dunia Imam Khomeini Mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Idadi kubwa ya Wairani kutoka matabaka mbalimbali ya kijamii na waumini wengi kutoka nchi nyingine duniani wameshiriki marasimu haya tajwa katika haram la Imam Khomeini kusini mwa Tehran huku waombolezaji wakitoa heshima kwa msanifu huyo Mapinduzi ya Kiislamu na kutangaza tena utiifu na kufungamana kwao na misingi na malengo ya Mapinduzi ya mwaka 1979.
Kiongozi Muadhamu amesema: Adui "mwovu" amepata kipigo na kufedheheka pakubwa katika makabiliano na majeshi ya Iran hiyo; na sasa anataka kufidia kushindwa kwake huko kupitia mkakati wa vita vya mseto.
Akiwahutubu wananchi, Ayatullah Mojtaba Khamenei amesema: "Adui hasidi, baada ya kushindwa pakubwa mbele ya vijana na watoto wenu shupavu katika Jeshi, na kupata fedheha kubwa katika medani ya vita na nambele ya macho ya walimwengu, sasa ameelekeza juhudi zake katika malengo mawili katika mfumo wa vita vya mseto: Mosi kuwakatisha tamaa wananchi na kuibua mahesabu khalati miongoni mwa maafisa wa nchi."
Akiendelea na ujumbe wake kwa mnasaba wa kumbukumbu ya mwaka wa 37 tangu kuaga dunia Imam Khomeini, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: Marasimu ya kumbukumbu ya kuaga dunia Imam Khomeini yanatoa fursa muhimu ya kutafakari na kumzingatia kwa makini "shakhsia huyu mashuhuri'.
Amemtaja hayati Imam kuwa shakhsia mwenye haiba, ambaye ufahamu wake wa kina na utambuzi wa njia na lengo lake tukufu utaangazia na kutoa mwanga wa mustakbali wa Iran ya Kiislamu.
Hata hivyo amesema, vijana wengi wa taifa hili hawajapata fursa ya kumfahamu moja kwa moja Hayati Imam Khomeini; na hata wengi kati ya wale walioishi enzi za uhai wake hawajafahamu kikamilifu undani wa shakhsia yake na misingi ya njia yake.
3497716