Takribani miaka 1376 iliyopita, ilifanyika majlisi ya kwanza ya siku ya Arubaini tangu kuuawa shahidi mjukuu wa Mtume Muhammad SAW Imam Hussein bin Ali AS akiwa na watu wa Nyumba Tukufu ya Mtume ambao waliuawa shahidi tarehe 10 Muharram mwaka 61 Hijria.
Habari ID: 3459320 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/12/02
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, jinai za kuogofya za makundi ya magaidi kama vile kukata vichwa na kuwachoma moto watu ni dalili ya kuwa mbali kabisa na Uislamu magaidi hao.
Habari ID: 3455805 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/11/22
Ayatullah Ahmad Khatami
Khatibu wa Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa wiki mjini Tehran amesema kundi la kigaidi la Daesh au ISIS matakfiri kwa ujumla ni mamluki wa Wazayuni ambao wametumwa kwa lengo la kuwagombanisha Waislamu.
Habari ID: 3454898 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/11/21
Rais Rouhani
Marais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Ufaransa wametangaza utayarifu wa nchi hizo mbili kwa ajili ya kushirikiana katika masuala ya usalama na habari za kipelelezi katika fremu ya mapambano dhidi ya ugaidi.
Habari ID: 3454175 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/11/18
Aplikesheni za kusoma Qur’ani Tukufu zinaendelea kupata umashuhuri katika nchi za Kiislamu na hata nchi zisizokuwa za Kiislamu kote duniani.
Habari ID: 3428150 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/11/01
Maulama na wasomi wakubwa walioshiriki katika kongamano la pili la kimataifa la 'Kuitafakari Qur'ani' lililomalizika nchini Morocco wamelaani vitendo vya ugaidi na makundi yenye misimamo mikali inayokinzana na mafundisho sahihi ya kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu.
Habari ID: 3421794 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/10/31
Tuko katika mwezi wa Muharram ambao unahuisha na kurejesha akilini kumbukumbu ya mapambano adhimu na yenye adhama. Muharram ni mwezi uliofungamana na jina la Hussein Ibn Ali (AS) na harakati isiyo na mbadala ya mtukufu huyo katika ardhi ya Karbala.
Habari ID: 3391638 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/10/22
Kampeni ya kusambaza zawadi za nakala za Qur'ani tukufu imezinduliwa Marekani na Baraza la Uhusiano wa Kiislamu Marekani CAIR katika kujibu matamshi yenye chuki dhidi ya Uislamu ya Ben Carson, anayetaka kugombea kiti cha urais nchini humo mwakani kwa tikiti ya chama cha Republican.
Habari ID: 3366378 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/09/22
Maulamaa Waislamu Ghana
Maulamaa wa Kiislamu nchini Ghana wametangaza msimamo wa kupinga vikali kundi la kigaidi la Daesh au ISIS na kutoa wito kwa vijana nchini humo kuisoma na kufahamu ipasavyo tafsiri ya Qur'ani kwa njia sahihi ili wasitumbukie katika mtego muovu wa ISIS.
Habari ID: 3360612 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/09/08
Kongamano la kimataifa la "Uislamu, Rehema kwa Dunia" litafanyika Jakarta, Indonesia kuanzia Oktoba 13-16.
Habari ID: 3360473 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/09/08
Katika jitihada za kupunguza ongezeko la ubaguzi na chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu huko Malawi, jamii ya Waislamu nchini humo imeanzisha jitihada za kuwezesha vyombo vya habari kupata maelezo sahihi kuhusu Uislamu.
Habari ID: 3359965 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/09/07
Magaidi wa Boko Haram hawawezi hata kusoma Qur'ani Tukufu wala kutekeleza maundisho ya dini ambayo wanadai kupigania wanapotekeleza jinai zao, amesema afisa mwandamizi wa jeshi la Nigeria.
Habari ID: 3355686 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/08/31
Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran ameelezea masikitiko yake kuhusu kimya cha Umoja wa Mataifa na taasisi zingine za kimataifa kuhusu mauaji yanayoendelea dhidi ya watu wasio na hatia nchini Yemen.
Habari ID: 3353340 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/08/29
Inakadiriwa kuwa Waislamu wasiopungua milioni nne wameuawa katika miongo ya hivi karibuni Mashariki ya Kati katika vita vilivyoanzisha na madola ya maghairbi hasa Marekani na Marekani na Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi NATO.
Habari ID: 3350564 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/08/23
Shule ya Qur'ani na Sayansi za Qur'ani imefunguliwa nchini Ghana kwa hisani ya Taasisi ya Sheikh Eid ya Misaada ya Qatar.
Habari ID: 3349417 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/08/20
TEHRAN (IQNA)- Mwezi moja baada ya kutangaza kuikumbatia dini tukufu ya Kiislamu, Emmanuel Adebayor, mchezaji soka mashuhuri Mwafrika nchini Uingereza ambaye sasa ni mshambuliaji wa Tottenham, amefafanua sababu zilizompelekea kusilimu.
Habari ID: 3338997 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/08/04
Waislamu nchini Marekani wameanzisha kampeni yenye lengo la kuonesha sura sahini na adhimu ya Mtukufu Mtume Muhammad SAW kwa wafuasi wa dini nyingine duniani.
Habari ID: 3316510 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/06/20
Watu 183 waliosilimu na wanaoishi Qatar wamejisajilisha kushiriki katika mashindano ya kitaifa ya Qur’ani katika nchi hiyo ya Ghuba ya Uajemi.
Habari ID: 3313858 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/06/13
Katika siku za kukaribia tarehe 27 Rajab Mohammad SAW alikuwa akienda katika pango la Hiraa na katika baadhi ya nyakati alikuwa akikaa siku kadhaa katikaeneo hilo. Alikuwa akimfahamisha mke wake mtiifu Khadija kuwa: ‘Wewe pia wafahamu mahaba na mafungamano yangu. Katika siku hizi nina hisia ya ajabu ya kupenda kumkumbuka Mola muumba, moyo wangu hautaki chochote isipokuwa hilo.’
Habari ID: 3303983 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/05/15
Shirika la Mawasiliano na Utamaduni wa Kiislamu Iran (ICRO) limetayarisha tarjama ya Barua ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa lugha 21 duniani.
Habari ID: 2910931 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/02/28