uislamu - Ukurasa 8

IQNA

Shule ya Qur'ani na Sayansi za Qur'ani imefunguliwa nchini Ghana kwa hisani ya Taasisi ya Sheikh Eid ya Misaada ya Qatar.
Habari ID: 3349417   Tarehe ya kuchapishwa : 2015/08/20

TEHRAN (IQNA)- Mwezi moja baada ya kutangaza kuikumbatia dini tukufu ya Kiislamu, Emmanuel Adebayor, mchezaji soka mashuhuri Mwafrika nchini Uingereza ambaye sasa ni mshambuliaji wa Tottenham, amefafanua sababu zilizompelekea kusilimu.
Habari ID: 3338997   Tarehe ya kuchapishwa : 2015/08/04

Waislamu nchini Marekani wameanzisha kampeni yenye lengo la kuonesha sura sahini na adhimu ya Mtukufu Mtume Muhammad SAW kwa wafuasi wa dini nyingine duniani.
Habari ID: 3316510   Tarehe ya kuchapishwa : 2015/06/20

Watu 183 waliosilimu na wanaoishi Qatar wamejisajilisha kushiriki katika mashindano ya kitaifa ya Qur’ani katika nchi hiyo ya Ghuba ya Uajemi.
Habari ID: 3313858   Tarehe ya kuchapishwa : 2015/06/13

Katika siku za kukaribia tarehe 27 Rajab Mohammad SAW alikuwa akienda katika pango la Hiraa na katika baadhi ya nyakati alikuwa akikaa siku kadhaa katikaeneo hilo. Alikuwa akimfahamisha mke wake mtiifu Khadija kuwa: ‘Wewe pia wafahamu mahaba na mafungamano yangu. Katika siku hizi nina hisia ya ajabu ya kupenda kumkumbuka Mola muumba, moyo wangu hautaki chochote isipokuwa hilo.’
Habari ID: 3303983   Tarehe ya kuchapishwa : 2015/05/15

Shirika la Mawasiliano na Utamaduni wa Kiislamu Iran (ICRO) limetayarisha tarjama ya Barua ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa lugha 21 duniani.
Habari ID: 2910931   Tarehe ya kuchapishwa : 2015/02/28

Kiongozi wa Chuo Kikuu cha al-Azhar nchini Misri Ahmad al-Tayib, ametoa wito kwa nchi za Kiislamu kufanyia marekebisho mitalaa ya elimu katika taasisi za elimu ili kupunguza wimbi la vijana kujiunga na makundi ya kigaidi.
Habari ID: 2891633   Tarehe ya kuchapishwa : 2015/02/24

Rais Barack Obama wa Marekani amesema kuwa, nchi hiyo haina vita na Uislamu, bali inapambana na watu wanaoupotosha Uislamu.
Habari ID: 2876869   Tarehe ya kuchapishwa : 2015/02/21

Sayyid Hassan Nasrullah
Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, harakati za kundi la kitakfiri na kigaidi la Daesh (ISIS) zinatekeleza kikamilifu malengo ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 2862976   Tarehe ya kuchapishwa : 2015/02/17

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, mafundisho ya dini tukufu ya Kiislamu yanatuamrisha kuamiliana vyema, kwa insafu na uadilifu na wafuasi wa dini nyinginezo za mbinguni.
Habari ID: 2862975   Tarehe ya kuchapishwa : 2015/02/17

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema malengo na misingi ya Mapinduzi ya Kiislamu haiwezi kubadilika.
Habari ID: 2840031   Tarehe ya kuchapishwa : 2015/02/11

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amemuandikia barua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban-Ki moon ambapo mbali na kulaani vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu ameambatanisha barua ya hivi karibuni ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa vijana wa Ulaya na Amerika ya Kaskazini.
Habari ID: 2822425   Tarehe ya kuchapishwa : 2015/02/08

Mchezaji soka nchini Ujerumani Danny Blum ametangaza kusilimu na kuutaja Uislamu kuwa dini ya matumaini na nguvu.
Habari ID: 2779913   Tarehe ya kuchapishwa : 2015/01/29

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa maafa makubwa yanayofanywa na makundi ya kigaidi kama lile la Boko Haram yanaathiri na kuumiza sana dhamira za wanadamu kote dunia.
Habari ID: 2771315   Tarehe ya kuchapishwa : 2015/01/27

Waislamu na hata wasiokuwa Waislamu duniani wanaendelea kulaani kitendo cha hivi karibuni cha jarida moja la Ufaransa la Charlie Hebdo kuchora vibonzo vinavyomvunjia heshima Mtumu Mtukufu wa Uislamu, Mohammad SAW.
Habari ID: 2766561   Tarehe ya kuchapishwa : 2015/01/26

Imam Khamenei
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa ujumbe kwa vijana wa Ulaya na Amerika Kaskazini akisema kuwa, matukio ya hivi karibuni nchini Ufaransa na matukio yanayoshabihiana na hilo katika baadhi ya nchi za Magharibi yamemlazimisha azungumze nao moja kwa moja.
Habari ID: 2747324   Tarehe ya kuchapishwa : 2015/01/22

Kansela wa Ujerumani Bi Angela Markel amesema kuwa, Waislamu wanaoishi nchini humo ni .miongoni mwa jamii ya Wajerumani
Habari ID: 2706291   Tarehe ya kuchapishwa : 2015/01/13

Kutokana na ongezeko kubwa la chuki dhidi ya Waislamu na Uislamu huko Malawi, Waislamu nchini humo wameanzisha kampeni ya kuwashawishi wafuasi wa dini nyinginezo kuzingatia msingi wa ‘kuishi pamoja kwa amani’ ili kuzuia uwezekano wa kuibuka malumbano ya kidini katika nchi hiyo ya kusini wa Afrika.
Habari ID: 2621819   Tarehe ya kuchapishwa : 2014/12/18

Kongamano la Kimataifa la Kupambana na Ugaidi na Uchupaji Mipaka lililokuwa likifanyika katika taasisi ya al Azhar nchini Misri limesisitiza katika taarifa yake ya mwisho kuwa, makundi ya kitakfiri na yenye misimamo mikali hayana uhusiano wowote na Uislamu.
Habari ID: 2615265   Tarehe ya kuchapishwa : 2014/12/05

Utafiti umeonesha kuwa, jina la Muhammad linaongoza kuitwa watoto nchini Uingereza, ambapo jina hilo limeonekana kupewa watoto wengi zaidi wa kiume kati ya waliozaliwa mwaka huu wa 2014 nchini humo.
Habari ID: 2614518   Tarehe ya kuchapishwa : 2014/12/02