waislamu - Ukurasa 27

IQNA

TEHRAN (IQNA)- Umoja wa Afrika (AU) umesimamisha nafasi ya mwanachama mwangalizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika umoja huo hatua ambayo ni pigo kwa utawala huo unaokaliwa kwa mabavu ardhi za Palestina.
Habari ID: 3474901   Tarehe ya kuchapishwa : 2022/02/07

TEHRAN (IQNA)- Msikiti mmoja katika mji mkuu wa Austira, Vienna umehujumiwa na watu wasiojulikana ikiwa ni ongezeko la chuki dhidi ya Uislamu barani Ulaya.
Habari ID: 3474893   Tarehe ya kuchapishwa : 2022/02/05

TEHRAN (IQNA)- Wanawake Waislamu wanaohudumu katika Kikosi cha Gadi ya Pwani ya Ufilipino sasa wanaruhusiwa kuvaa Hijabu ikiwa ni katika jitihada za kuwahimiza wanawake Waislamu wajiunge na kikosi hicho.
Habari ID: 3474888   Tarehe ya kuchapishwa : 2022/02/04

TEHRAN (IQNA) – Kituo cha Kiislamu cha Al Azhar nchini Misri kimepongeza uamuzi wa serikali ya Canada kutangaza siku maalumu ya kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu.
Habari ID: 3474879   Tarehe ya kuchapishwa : 2022/02/01

TEHRAN (IQNA)- Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet ameitaka jamii ya kimataifa izidishe mashinikizo kwa jeshi la Myanmar ili likomeshe kampeni yake ya ukatili na ukandamizaji dhidi ya watu wa Myanmar na kusisitiza kurejeshwa mara moja utawala wa kiraia nchini humo.
Habari ID: 3474869   Tarehe ya kuchapishwa : 2022/01/30

TEHRAN (IQNA)- Waziri Mkuu wa Pakistan Imran Khan amempongeza mwenzake wa Canada kutokana na hatua yake ya kulaani chuki dhidi ya Uislamu yaani Islamophobia huku akitaka kuwepo jitihada maalumu za kukabiliana na tatizo hilo.
Habari ID: 3474868   Tarehe ya kuchapishwa : 2022/01/30

TEHRAN (IQNA)-Nakala ya majaribio ya Qur'ani Tukufu iliyoandikwa kwa maandishi ya nukta nundu (braille) katika Kituo cha Kiislamu cha Al Azhar imezinduliwa katika Maoneysho ya Kimataifa ya Vitabu ya Cairo.
Habari ID: 3474859   Tarehe ya kuchapishwa : 2022/01/28

TEHRAN (IQNA)- Wanafuzni Waislamu katika Shule ya Upili ya Park High mtaa wa Stanmore nchini London wanasema mwalimu mmoja shuleni hapo amewanyima idhini ya kusali Sala ya Ijumaa katika uwanja wa shule.
Habari ID: 3474857   Tarehe ya kuchapishwa : 2022/01/26

TEHRAN (IQNA)- Kadhia ya chuki dhidi ya Uislamu na kubaguliwa Waislamu katika nchi za Ulaya ikiwemo Uingereza imeshika kasi katika miaka ya hivi karibuni. Chuki hizi dhidi ya Uislamu sasa zimefika hata katika ngazi rasmi za serikali.
Habari ID: 3474845   Tarehe ya kuchapishwa : 2022/01/24

TEHRAN (IQNA)- Kituo cha zamani cha polisi katika mji wa Cardiff eneo la Wales nchini Uingereza kitabadilishwa kuwa msikiti.
Habari ID: 3474840   Tarehe ya kuchapishwa : 2022/01/23

TEHRAN (IQNA)- Baraza la Seneti la Ufaransa limepiga kura na kuidhnisha sheria inayopiga marufuku wanawake Waislamu kuvaa vazi la stara na heshima la Hijabu katika mashindano ya michezo.
Habari ID: 3474830   Tarehe ya kuchapishwa : 2022/01/20

TEHRAN (IQNA)- Mfanya biashara mwanamke Muislamu Mjamaica ametoa wito kwa serikali ya nchi hiyo kutekeleza sera ya kutowabagua wanawake Waislamu maeneo ya kazi na vituo vya elimu sambamba na kulinda haki zao.
Habari ID: 3474822   Tarehe ya kuchapishwa : 2022/01/18

TEHRAN (IQNA)- Waislamu katika eneo la Ufilipino lenye mamlaka ya ndani la Bangsamoro wanaadihimisha mwaka wa tatu tokea wapate mamlaka ya dani ya kujitawala.
Habari ID: 3474821   Tarehe ya kuchapishwa : 2022/01/18

TEHRAN (IQNA) – Mashindano ya 17 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Algeria yatafanyika kwa njia ya intaneti, imetangaza Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kidini nchini humo.
Habari ID: 3474803   Tarehe ya kuchapishwa : 2022/01/13

TEHRAN (IQNA) - Makumi ya walowezi wa Kizayuni wameuvamia tena msikiti wa al-Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) ambapo wameuvunjia heshima msikiti huo ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu.
Habari ID: 3474794   Tarehe ya kuchapishwa : 2022/01/11

TEHRAN (IQNA)-Serikali ya Ufaransa imevunja Baraza la Fiqhi la Waislamu wa Ufaransa (CFCM) ikiwa ni muendelezo wa sera zake za kuwakandamiza Waislamu.
Habari ID: 3474793   Tarehe ya kuchapishwa : 2022/01/11

TEHRAN (IQNA)- Viongozi wa Kiislamu na Kikristo nchini Cameroon wameshiriki katika dua ya pamoja kuomba amani na mafanikio ya mashindano ya soka ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).
Habari ID: 3474781   Tarehe ya kuchapishwa : 2022/01/08

TEHRAN (IQNA)- Mwanazuoni maarufu wa Nigeria na muasisi wa Taasisi ya Darul Hadith ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 79.
Habari ID: 3474779   Tarehe ya kuchapishwa : 2022/01/07

TEHRAN (IQNA)- Waislamu nchini Marekani wanataka uchunguzi ufanyike baada ya msikiti kuhujumiwa katika mji wa Waterloo jimboni Iowa.
Habari ID: 3474775   Tarehe ya kuchapishwa : 2022/01/06

TEHRAN (IQNA) – Waislamu nchini Ghana wameshiriki kikao cha kusoma Qur’ani kwa ajili ya kuomba baraka za Allah SWT.
Habari ID: 3474772   Tarehe ya kuchapishwa : 2022/01/06