waislamu - Ukurasa 30

IQNA

TEHRAN (IQNA)- Kiongozi wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amelaani vikali hujuma ya hivi karibuni ya wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya nyumba ya Sheikh Ikrima Sabri na kusisitiza kuhusu mshikamano wa Wapalestina katika kutetea Mji wa Quds (Jerusalem) na Msikiti wa Al Aqsa ulio mjini humo.
Habari ID: 3474409    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/10/11

Mnamo 14 Dhul Hija 1442 Hijria Qamaria sawa na 25 Julai 2021, Waislamu wa Afrika Mashariki na maeneo mengine duniani walikumbwa na majonzi kufuatia kuaga dunia mwanazuoni mtajika wa Kiislamu na mfasiri wa Qur’ani Tukufu Alhaj Sheikh Hassan Mwalupa.
Habari ID: 3474408    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/10/10

TEHRAN (IQNA)- Umoja wa Mataifa umetia saini mapatano na Bangladesh kuhusu kuwasiadia wakimbizi Waislamu wa jamii ya Rohingya ambao wako katika kisiwa kimoka cha Ghuba ya Bengal.
Habari ID: 3474407    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/10/10

Kiongozi Muadhamu katika ujumbe kufuatia hujuma ya kigaidi msikitini Afghanistan
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ametoa mwito kwa mamlaka za Kabul kuwaadhibu waliohusika na shambulizi la bomu lililoua makumi ya watu msikitini katika mji wa Kunduz nchini Afghanistan juzi Ijumaa.
Habari ID: 3474404    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/10/10

TEHRAN (IQNA)- Kituo cha Kiislamu cha Al Azhar Misri na Mufti Mkuu nchini humo wametoa taarifa na kulaani vikali hujuma ya kigaidi ya Ijumaa dhidi ya Msikiti wa Waislamu wa Madhehebu ya Shia ambapo watu takribani 100 wameuawa.
Habari ID: 3474399    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/10/09

TEHRAN (IQNA)- Mfanyakazi wa zamani wa mtandao wa Facebook amesema shirika hilo la Kimarekani lilipuuza kwa makusudi taaraifa zilizo na chuki dhidi ya Waislamu ambazo zilikuwa zikienezwa katika mtandao huo nchini India.
Habari ID: 3474396    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/10/08

TEHRAN (IQNA)- Afisa mmoja wa ngazi za juu nchini Malaysia amesedma nchi za Afrika zinaweza kunufaika na soko kubwa la sekta ya chakula ‘Halal’ duniani yenye thamani ya dola bilioni 739.
Habari ID: 3474393    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/10/07

TEHRAN (IQNA)- Wahindi wenye misimamo mikali katika jimbo la Assam nchini India wameshadidisha hujuma dhidi ya Waislamu eneo hilo.
Habari ID: 3474389    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/10/06

TEHRAN (IQNA)- Baraza Kuu la Waislamu Fiji limetangaza kuwa misikiti itafunguliwa tena nchini humo kuanzia Oktoba nne lakini watakaoruhusiwa ni wale tu waliopata chanjo kamili ya COVID-19 au corona.
Habari ID: 3474371    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/10/02

TEHRAN (IQNA)- Mmoja wa viongozi wa jamii ya Waislamu wa Rohingya waliokimbilia Bangladesh kutoka Myanmar ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana.
Habari ID: 3474370    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/10/02

TEHRAN (IQNA)- Idadi ya Waislamu watakaruhusiwa kutekelelza Hija ndogo au Umrah na kuswali katika Msikiti Mtakatifu wa Makka (Masjid al-Haram) imeongezeka hadi laki moja kwa siku kuanzia Oktoba Mosi.
Habari ID: 3474369    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/10/01

TEHRAN (IQNA)- Mufti Mkuu wa Oman Sheikh Ahmed bin Hamad Al-Khalili ametoa wito kwa Ummah wa Kiislamu duniani kuungana na kuwatetea Waislamu wa India.
Habari ID: 3474358    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/09/29

TEHRAN (IQNA)- Kongamano la Kimataifa la ‘Arubaini, Umaanawi na Fadhila za Kiakhlaqi’ limefanyika katika mji wa Karbala.
Habari ID: 3474354    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/09/28

TEHRAN (IQNA)- Mkutano mkuu wa chama cha Leba nchini Uingereza umepigia kura na kupitisha hoja ya kuitambua Israel kuwa ni utawala unaotenda jinai ya ubaguzi wa Apathaidi, na kukifanya kuwa chama cha kwanza kikubwa cha siasa barani Ulaya kuchukua msimamo huo dhidi ya utawala haramu wa Kizayuni.
Habari ID: 3474349    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/09/27

TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amezungumzia hujuma za kipropaganda zinazofanywa na maadui dhidi ya taifa la Iran kwa ajili ya kushawishi fikra za watu kwa kutumia mbinu na nyenzo mbalimbali na kusema harakati za kutoa ufafanuzi na kueleza haki zinazima hujuma hizo za kipropaganda.
Habari ID: 3474348    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/09/27

TEHRAN (IQNA)- Waislamu wa jamii ya Wauyghur Waturuki wanaoishi katika mji wa Toronto, Canada wamenunua jengo la kale ambalo lilikuwa Kanisa na kuligeuza kuwa Msikiti.
Habari ID: 3474344    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/09/26

TEHRAN (IQNA)- Jumuiya ya Madaktari wa Kiislamu Pakistan (PIMA) inapanga kuandaa warsha za kuokoa maisha kwa wananchi katika misikiti kote Pakistan.
Habari ID: 3474339    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/09/25

TEHRAN (IQNA)- Eneo la kiviwanda la Turin, ambao ni kati ya miji mikubwa Italia, hivi karibuni litakua na fahari ya kupata kituo kikubwa cha utamaduni wa Kiislamu ambacho kitajumuisha pia msikiti.
Habari ID: 3474332    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/09/23

TEHRAN (IQNA)- Mwanamke mmoja Muislamu katika jimbo la Michigan nchini Marekani amelalamika kuwa polisi walimvua Hijabu baada ya kumkamata. Alivuliwa Hijabu katika kituo cha polisi wakati wa kupigwa picha.
Habari ID: 3474319    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/09/20

TEHRAN (IQNA) – Darul Iftaa ya Misri imetangaza marufuku ya kuandika aya za Qur'ani Tukufu kwa alfabeti za kilatini.
Habari ID: 3474316    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/09/20