waislamu - Ukurasa 28

IQNA

TEHRAN (IQNA)- Video zinazowaonyesha viongozi wa kidini wa Kihindu nchini India wakitoa wito wa mauaji ya halaiki dhidi ya Waislamu zimezua hasira na wito madai ya kuchukuliwa hatua dhidi ya wahusika.
Habari ID: 3474719   Tarehe ya kuchapishwa : 2021/12/25

TEHRAN (IQNA) – Jumuiya ya Waislamu Windsor wanatafakari kufungua kesi katika Mahakama Kuu ya Uingereza baada ya kunyimwa idhini ya kujenga msikiti katika mji wa Windsor.
Habari ID: 3474683   Tarehe ya kuchapishwa : 2021/12/16

TEHRAN (IQNA)- Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Tatarstan katika Shirikisho la Russia, Marat Khusnullin, ameidhinisha mpango wa kusherehekea mwaka wa 1,100 tokea Uislamu uingie eneo hilo.
Habari ID: 3474682   Tarehe ya kuchapishwa : 2021/12/16

TEHRAN (IQNA)- Ubelgiji imeondoa marufuku ya uvaaji vazi la stara ya mwanamke wa Kiislamu Hijabu iliyokuwa imewekwa kwa wale wanaoingia katika mahakama za nchi hiyo.
Habari ID: 3474677   Tarehe ya kuchapishwa : 2021/12/15

TEHRAN (IQNA)- Polisi nchini Canada imemkamata mtu mmoja Jumatatu baada ya mzoga kutupwa nje ya msikiti katika eneo la Vaudreuil-Dorion hivi karibuni.
Habari ID: 3474674   Tarehe ya kuchapishwa : 2021/12/14

TEHRAN (IQNA)- Makaburi ya Waislamu katika mji wa Mulhouse, mashariki mwa Ufaransa yamehujumiwa na watu wasiojulikana Jumapili jioni.
Habari ID: 3474673   Tarehe ya kuchapishwa : 2021/12/14

TEHRAN (IQNA)- Mufti wa Mji wa Quds (Jerusalem) na Palestina amelaani vikali matamshi ya mbunge mmoja nchini Marekani ambaye ametaka Msikiti wa Al Aqsa mjini Quds uvunjwe.
Habari ID: 3474671   Tarehe ya kuchapishwa : 2021/12/14

TEHRAN (IQNA)- Mahafali ya kuhitimu mamia ya wanafunzi walioifadhi Qur'ani Tukufu imefanyika kaskazini mashariki mwa Uturuki katika mkoa wa Rize.
Habari ID: 3474668   Tarehe ya kuchapishwa : 2021/12/12

TEHRAN (IQNA)- Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema sera za ujirani mwema na kuwa na uhusiano na majirani ili kusambaratisha vikwazo ni mkakati wa kistratijia wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Habari ID: 3474666   Tarehe ya kuchapishwa : 2021/12/11

TEHRAN (IQNA)- Ofisi ya Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau imetangaza kuchukua hatua za kisheria dhidi ya sheria ya jimbo la Quebec ambayo imepelekea mwalimu mmoja Muislamu ahamishwe kazi kwa sababu tu alikuwa amevaa Hijabu.
Habari ID: 3474665   Tarehe ya kuchapishwa : 2021/12/11

TEHRAN (IQNA) – Sera rasmi ya serikali ya Ufaransa ya kubana uhuru wa Waislamu sasa imefika kiasi ambacho hakiwezi kustahamiliwa tena.
Habari ID: 3474655   Tarehe ya kuchapishwa : 2021/12/08

TEHRAN (IQNA)- Wanafuzni Waislamu katika Chuo Kikuu cha Kyambogo mjini Kampala nchini Uganda wanataka chuo hicho kiwaajiri maafisa usalama wanawake wanawake ambao watakua na jukumu la kuwapekua wanafunzi wa kike.
Habari ID: 3474654   Tarehe ya kuchapishwa : 2021/12/08

TEHRAN (IQNA)- Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria, Sheikh Ibrahim Zakzaky amezungumza kwa mnasaba wa maadhimisho ya mwaka wa sita wa kumbukumbu ya mauaji ya halaiki yaliyotekelezwa na jeshi la nchi hiyo katika mji wa Zaria jimboni Kaduna, dhidi ya wanachama wa harakati hiyo.
Habari ID: 3474642   Tarehe ya kuchapishwa : 2021/12/05

Hujjatul Islam Shahriyari
TEHRAN (IQNA)- Hujjatul Islam wal Muslimin Shahriari amesema itikadi ya Ukufurishaji ni kati ya njama za mabeberu na Wazayuni dhidi ya Uislamu.
Habari ID: 3474640   Tarehe ya kuchapishwa : 2021/12/04

TEHRAN (IQNA)- Wizara ya Wakfu ya Misri imeandaa mkutano wa kuchunguza hatua ambazo zinapaswa kuchukuliwa kwa ajili ya kuandaa Duruy a 28 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani.
Habari ID: 3474628   Tarehe ya kuchapishwa : 2021/12/02

TEHRAN (IQNA) – Mwanae qarii mashuhuri wa Qur’ani kutoka Misri Sheikh Abdul Basit Abdulswamad amesema baba yake alikuwa na sauti ambayo mbali na Waislamu inawavutia pia wasiokuwa Waislamu.
Habari ID: 3474626   Tarehe ya kuchapishwa : 2021/12/01

TEHRAN (IQNA) – Mbunge Muslamu katika Bunge la Congress nchini Marekani, Bi. Ilhan Omar wa chama cha Democrat amehujumiwa kwa maneno makali na mbunge mwenzake mwenye misimamo mikali wa chama cha Republican ambaye amemtaja kuwa ‘mwenye kiu cha damu’ na mtetezi wa ugaidi.
Habari ID: 3474624   Tarehe ya kuchapishwa : 2021/12/01

Msomi wa Lebanon
TEHRAN (IQNA)- Mwanazuoni maarufu wa Kiislamu nchini Lebanon amesema kuna haja ya kupitishwa sheria za kimataifa ambazo zinapiga marufuku uibuaji mifarakano na migongano baina ya wafuasi wa madhehebu mbali mbali za Kiislamu.
Habari ID: 3474620   Tarehe ya kuchapishwa : 2021/11/30

TEHRAN (IQNA)- Baraza la Jamii za Waislamu Duniani limeakhirisha Kongamano la Kimataifa la Umoja wa Kiislamu la Umoja wa Falme za Kiarabu baada ya kuibuka aina mpya ya kirusi cha COVID-19 ijulikanayo kama Omicron.
Habari ID: 3474618   Tarehe ya kuchapishwa : 2021/11/29

TEHRAN (IQNA)- Msikiti wa Imam Ali huko Ponta Grossa nchini Brazil umehujumiwa Ijumaa na watu wenye chuki dhidi ya Uislamu, wametangaza wasimamizi wa msikiti huo.
Habari ID: 3474615   Tarehe ya kuchapishwa : 2021/11/29