iqna

IQNA

Watetezi wa Qur'ani Tukufu
TEHRAN (IQNA) - Msomi wa Malaysia anasema ili kujibu kiuchumi mashambulizi ya Wamagharibi dhidi ya Uislamu na Qur'ani Tukufu, mataifa ya Kiislamu yanahitaji kuelewa uwezo wao na kujenga umoja.
Habari ID: 3477373    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/08/03

Watetezi wa Qur'ani
TEHRAN (IQNA) – Washiriki katika kongamano la kimataifa ambalo limeitishwa kujadili njia za kukabiliana na kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu wamesisitiza haja ya ulimwengu wa Kiislamu kuwa na umoja na mshikamano wa uhakika ili kkukabiliana na vitendo hivyo vya kufuru.
Habari ID: 3477372    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/08/02

Watetezi wa Qur'ani
TEHRAN (IQNA)- Kwa mara nyingine tena Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amelaani vitendo vya karibuni vya kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu katika nchi za Sweden na Denmark na kusisitiza kuwa, vitendo hivyo vya kudhalilisha matukufu ya kidini havina tofauti na ukatili.
Habari ID: 3477371    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/08/02

Watetezi wa Qur'ani
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amewataka vijana wote wa Kiislamu wasisubiri kauli za jumuiya na mashirika bali wachukue hatua ya kulipiza kisasi dhidi ya mtu aliyeichoma moto Qur'ani.
Habari ID: 3477370    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/08/02

Watetezi wa Qur'ani Tukufu
TEHRAN (IQNA)- Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Hossein Amir Abdollahian amewasilisha mapendekezo ya Iran kwa ajili ya kukabiliana na vitendo vya kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu katika nchi za Ulaya.
Habari ID: 3477369    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/08/01

Watetezi wa Qur'ani Tukufu
TEHRAN (IQNA)- Sheikh wa Al-Azhar wa nchini Misri, akijibu barua ya mkuu wa vyuo vya kidini vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ameeleza matumaini yake kuwa msimamo wa pamoja uliochukuliwa na Waislamu hivi karibuni katika kukabiliana na suala la kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu utakuwa kichocheo cha kutatua tofauti na kuleta umoja baina yao.
Habari ID: 3477367    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/08/01

Watetezi wa Qur'ani Tukufu
CAIRO (IQNA) - Semina itaandaliwa na Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar cha Misri kujadili kukabiliana na uhalifu wa uchomaji moto wa Qur'ani Tukufu katika nchi za Magharibi.
Habari ID: 3477366    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/08/01

Watetezi wa Qur'ani Tukufu
STOCKHOLM (IQNA) - Mwanazuoni wa Kiislamu mwenye makazi yake nchini Uswidi anasema vitendo vya mara kwa mara vya kuvunjiwa heshima Qur'ani katika nchi hiyo ya eneo la Nordic barani Ulaya vinaiweka sura ya Uswidi hatarini.
Habari ID: 3477360    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/30

Watetezi wa Qur'ani Tukufu
TEHRAN (IQNA) – Mwanaharakati wa kisiasa na haki za binadamu wa Bahrain amependekeza kwamba muungano wa taasisi za kiraia katika nchi za Kiislamu na zisizo za Kiislamu uanzishwe ili kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu na kuvunjiwa heshima matakatifu ya Kiislamu.
Habari ID: 3477359    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/30

Watetezi wa Qur'ani Tukufu
TEHRAN (IQNA) - Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA) litaandaa kongamano la mtandaoni kujadili kudhalilishwa kwa Qur'ani Tukufu kwa mtazamo wa haki za binadamu.
Habari ID: 3477354    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/29

Watetezi wa Qur'ani Tukufu
BEIRUT (IQNA)- Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema jamii za Kiislamu haiwezi kustahamili kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu, akisisitiza kwamba Waislamu wako tayari kikamilifu kuchukua hatua za kuwajibika kuulinda Uislamu na kitabu chao kitakatifu.
Habari ID: 3477352    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/29

Watetezi wa Qur'ani Tukufu
BAGHDAD (IQNA) - Washiriki katika mkutano wa kutetea Qur'ani Tukufu nchini Iraq wamesisitiza haja ya kutunga sheria za kimataifa zinazoharamisha kuvunjiwa heshima matakatifu ya kidini.
Habari ID: 3477350    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/28

Watetezi wa Qur'ani Tukufu
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameijibu barua aliyoandikiwa na Kiongozi wa juu wa kidini wa Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Iraq kuhusu kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu katika nchi za Uswidi na Denmark.
Habari ID: 3477349    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/28

Watetetezi wa Qur'ani Tukufu
SANAA (IQNA) - Maandamano makubwa yalifanyika Sana'a, mji mkuu wa Yemen, kulaani unajisi wa hivi majuzi wa maeneo matakatifu ya Kiislamu nchini Uswidi na Denmark.
Habari ID: 3477346    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/26

Watetezi wa Qur'ani Tukufu
CAIRO (IQNA) - Kufuatia matukio ya mara kwa mara ya kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu nchini Uswidi na Denmark, Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar cha Misri kimetoa wito kwa Waislamu na nchi za Kiislamu kususia bidhaa za nchi hizo mbili za Ulaya.
Habari ID: 3477345    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/26

Watetezi wa Qur'ani Tukufu
NEW YORK (IQNA) – Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Jumanne lilipitisha azimio la kulaani aina zote za kuvunjiwa heshima vitabu vitakatifu likitambua vitendo vya aina hiyo kuwa ni ukiukaji wa sheria za kimataifa.
Habari ID: 3477341    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/26

Watetezi wa Qur'ani Tukufu
QATAR (IQNA) -Supamaketi kubwa nchini Qatar imeondoa bidhaa zote za Uswidi kwenye rafu zake - na kutoa msimamo wa kulaani kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu katika nchi hiyo ya Skandinavia, kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya ndani.
Habari ID: 3477340    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/25

Watetezi wa Qur'ani Tukufu
TEHRAN (IQNA)- Waislamu wa Ghana wametoa wito wa kufanyika maandamano ya kimataifa ya kulaani uchomaji wa Qur'ani wakati huu wa maombolezo ya Muharram.
Habari ID: 3477339    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/25

Watetezi wa Qur'ani Tukufu
TEHRAN (IQNA)-Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa kutoa leseni ya kuidhalilisha na kuivunjia heshima Qur'ani Tukufu ni kinyume na madai ya uhuru wa kusema na ni kielelezo cha "ujinga mamboleo".
Habari ID: 3477331    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/24

Watetezi wa Qur'ani Tukufu
TEHRAN (IQNA)- Waislamu katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo Iran, Iraq, Lebanon na Nigeria wamefanya maandamano makubwa na kulaani kitendo cha kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu nchini Sweden.
Habari ID: 3477329    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/24