TEHRAN (IQNA) –Malaysia imepewa jukumu la kutayarisha chakula halali, ambacho kimetayarishwa kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu, kwa ajili ya michezo ya Olimpiki ya Tokyo 2020.
Habari ID: 3472477 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/16
TEHRAN (IQNA) – Hatua ya kujiuzulu Sajid Javid, waziri Muislamu wa ngazi za juu zaidi katika chama tawala cha Kihafihdhina (Conservative) cha Uingereza imepelekea chama hicho kutuhumiwa kuwa kinachochea hisia za chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) .
Habari ID: 3472476 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/16
TEHRAN (IQNA) – Polisi nchini Ujerumani Ijumaa waliwakamata watu 12 ambao wanashukiwa kuanzisha mtandano wa mrengo wa kulia wenye misimamo mikali kwa lengo la kutekeleza hujuma dhidi ya wanasiasa, wakimbizi na Waislamu.
Habari ID: 3472472 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/15
Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu asema
TEHRAN (IQNA) - Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amemtaja Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha IRGC kama shakhsia aliyehuisha 'harakati za jihadi na kuuawa shahidi' katika ulimwengu wa Kiislamu.
Habari ID: 3472471 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/14
Sayyid Hassan Nasrallah
TEHRAN (IQNA) - Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kwa kumuua kigaidi shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani Kamanda wa Kikosi cha Qods cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), Marekani ilivuka mistari yote miekundu na kwamba mauaji hayo yamegeuza mahesabu yote katika eneo la Asia Magharibi.
Habari ID: 3472470 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/14
TEHRAN (IQNA) - Marasimu ya maombolezo ya arubaini ya shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani Kamanda wa Kikosi cha Qods cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) yamefanyika Alhamisi kote nchini Iran kwa kuhudhuriwa na umati mkubwa wa matabaka mbalimbali ya wananchi.
Habari ID: 3472469 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/14
TEHRAN (IQNA) - Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imetangaza orodha ya mashirika ambayo yanashirikiana na utawala wa Israel katika kujenga vitongoji haramu katika ardhi za Palestina huko Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
Habari ID: 3472468 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/13
TEHRAN (IQNA) – Makumi ya walowezi wa Kizayuni wameuhujumu Msikiti wa Al Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3472467 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/13
TEHRAN (IQNA) - "Iwapo utawala wa Kizayuni wa Israel utatekeleza uvamizi au hatua yoyote ya kijinga dhidi ya maslahi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Syria na katika eneo, basi utawala huo utapokea jibu kali ambalo litakuwa la majuto."
Habari ID: 3472466 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/13
TEHRAN (IQNA) - Msichana kutoka katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ametimiza ndoto yake ya kujenga msikiti katika nchi masikini.
Habari ID: 3472465 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/12
TEHRAN (IQNA) - Ismail Haniya Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amemtumia ujumbe Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na akimpongeza yeye na taifa la Iran kufuatia maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Habari ID: 3472463 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/12
TEHRAN (IQNA) - Mamilioni ya wananchi wa Iran wamejitokeza mabarabarani katika miji na vijiji vya nchi hii kushiriki matembezi ya Bahman 22, kwa mnasaba wa kutimia mwaka wa 41 wa Ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Habari ID: 3472462 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/11
Rais Hassan Rouhani
TEHRAN (IQNA) - Rais Hassan Rouhani amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaendelea kustawi na kuimarika licha ya uhasama na njama za maadui hususan Marekani, na kwamba 'Mapinduzi ya Kiislamu' lilikuwa chaguo la taifa zima la Iran.
Habari ID: 3472461 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/11
TEHRAN (IQNA) - Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amesema kuwa, mipango ya Marekani na utawala ghasibu wa Israel na ushirikiano wao mkubwa wa kutekeleza mpango wa Muamala wa Karne na kuchora ramani mpya ya kuliunganisha eneo la Ukingo wa Magharibi na ardhi zinazokaliwa kwa mabavu, utafeli na kushindwa.
Habari ID: 3472458 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/10
TEHRAN (IQNA) – Watu wasiojulikana wameuhujumu msikiti katika mji wa Ulm nchini Ujerumani katika tukio linalohesabiwa kuwa ni la chuki dhidi ya Uislamu.
Habari ID: 3472456 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/10
TEHRAN (IQNA) - Viongozi wa Afrika wameulaani mpango uliopendekezwa na Rais Donald Trump wa Marekani ambao ni maarufu kama 'muamala wa karne' kuhusu utatuzi wa mgogoro wa Israel na Palestina na kuutaja kuwa usio na uhalali.
Habari ID: 3472455 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/09
TEHRAN (IQNA) - Watu 26 wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa nchini Thailand baada ya kupigwa risasi kiholela na mwanajeshi mmoja wa nchi hiyo katika mji wa Nakhon Ratchasima.
Habari ID: 3472454 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/09
TEHRAN (IQNA) - Maandamano makubwa ya 22 Bahman (11 Februari) katika kuadhimisha ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu yamepangwa kufanyika katika miji na vijiji 5,200 kote Iran.
Habari ID: 3472453 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/09
AMIRI JESHI MKUU WA IRAN
TEHRAN (IQNA) - Amiri Jeshi Mkuu wa vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, kuna ulazima wa Iran kuwa na nguvu katika pande zote hasa katika uga wa ulinzi; na akasisitiza kwamba: "Ni lazima kuwa na nguvu ili vita visiibuke na vitisho viishe."
Habari ID: 3472451 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/08
TEHRAN (IQNA) - Waislamu wa Slovenia wameshiriki katika Sala ya kwanza ya Ijumaa katika msikiti pekee nchini humo.
Habari ID: 3472450 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/08