iqna

IQNA

TEHRAN (IQNA) – Misri imetangaza sheria ya kutotoka nje kuanzia saa moja usiku hadi saa kumi na mbili asubuhi kuanzia Jumatano kwa muda wa wiki mbili ili kukabiliana na kuenea kwa kasi uongjwa hatai wa COVID-19 maarufu kama corona.
Habari ID: 3472598    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/03/24

TEHRAN (IQNA) – Uongjwa wa COVID-19 maarufu kama corona umewaathiri Waislamu kote duniani hasa kutokana na kufungwa misikiti kwa muda ili kuzuia kuenea ugonjwa huo na hivi sasa viongozi wa Kiislamu wanabadilisha mbinu za kuwaongoza Waislamu kiroho.
Habari ID: 3472597    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/03/24

TEHRAN (IQNA) - Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amemuandikia barua Mfalme Salman wa Saudia na kusitiza juu ya ulazima wa kuachiliwa huru haraka iwezekanavyo wafungwa wa Kipalestina wanaoshikiliwa nchini Saudi Arabia.
Habari ID: 3472596    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/03/23

TEHRAN (IQNA) – Sala za jamaa zimesitishwa kwa muda katika Msikiti wa Al- Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa corona au COVID-19.
Habari ID: 3472595    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/03/23

TEHRAN (IQNA) – Saudi Arabia imeanza kutekeleza sheria ya kutotoka nje au curfew baada ya kuongezeka idadi ya watu walioambukizw augonjwa wa COVID-19 au corona nchini humo.
Habari ID: 3472594    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/03/23

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema Marekani haiaminiwi hata kidogo na kuongeza kuwa: "Wakati Marekani inatuhumiwa kutegeneza kirusi cha corona, ni mwanadamu yupi mwenye akili atakubali msaada wa nchi hiyo."
Habari ID: 3472592    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/03/22

TEHRAN (IQNA) - Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Kiislamu ya Palestina HAMAS usiku wa kuamkia leo amezungumza kwa simu na Mohammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu na kulaani vikali vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran.
Habari ID: 3472591    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/03/22

Rais wa Iran katika ujumbe maalumu wananchi wa Marekani
TEHRAN (IQNA) - Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewatumia ujumbe maalumu wananchi wa Marekani akitahadharisha kuwa: Siasa zozote za uono finyu na za uhasama zitazolenga kudhoofisha mfumo wa utabibu na kuviwekea mpaka vyanzo vya fedha vya kushughulikia hali mbaya iliyoko Iran zitakuwa na athari ya moja kwa moja kwa mchakato wa kupambana na janga la dunia nzima la corona katika nchi zingine.
Habari ID: 3472588    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/03/21

Zarif katika mhojiano na Folha de S.Paulo
TEHRAN (IQNA)- Waziri wa Mambo ya Nje wa amesema kuwa, ugaidi wa kimatibabu wa Marekani unatatiza mapambano athirifu dhidi ya maambukizi ya virusi hivyo vinavyoenea kwa kasi duniani.
Habari ID: 3472587    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/03/21

Sayyed Hassan Nasrallah
TEHRAN (IQNA) - Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema, maadui wanafanya kila njia ili kuyumbisha imani iliyopo baina ya Muqawama na wananchi, ambao ndio watoaji msukumo halisi kwa mhimili wa muqawama.
Habari ID: 3472586    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/03/21

TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametuma salamu za kheri na fanaka kwa munasaba wa kuwadia siku kuu ya Nowruz (Nairuzi) ya mwaka mpya wa Hijria Shamsia na wakati huo huo akatuma salamu za rambi rambi kutokana na kupoteza maisha idadi kubwa ya watu kutokana na ugonjwa wa COVID-19 au corona.
Habari ID: 3472585    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/03/20

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika ujumbe wa Nairuzi*
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameutaja mwaka mpya wa Kiirani wa 1399 Hijria Shamsia ulioanza leo nchini Iran kuwa ni Mwaka wa Ustawi Mkubwa katika Uzalishaji na kusema: Hatua kubwa ya uzalishaji inapaswa kuleta mabadiliko yanayohisika katika maisha ya wananchi.
Habari ID: 3472584    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/03/20

Rais Hassan Rouhani katika ujumbe wa Nairuzi*
TEHRAN (IQNA)- Rais Hassan Rouhani wa Iran ametuma ujumbe wa munasaba wa mwaka mpya wa Kiirani wa 1399 Hijria Shamsiya na kusema mwaka mpya utakuwa mwaka wa afya, ajira na ustawi wa kiuchumi na kiutamaduni nchini Iran.
Habari ID: 3472583    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/03/20

TEHRAN (IQNA) – Algeria imesitisha sala za Ijumaa na kufunga misikiti yote nchini humo kwa kama ikiwa ni katika jitihada za kuzuia kuenea ugonjwa wa COVID-19 maarufu kama corona.
Habari ID: 3472582    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/03/19

TEHRAN (IQNA) – Misikiti kadhaa muhimu katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi imefungwa kutokana na hofu ya kuenea ugonjwa wa COVID-19 maarufu kama kirusi cha corona.
Habari ID: 3472580    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/03/19

TEHRAN (IQNA) – Mwandishi habari Mmarekani anayeishi nchini Iran amesema anafadhilisha kubakia Iran wakati huu wa kuenea maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19 maarufu kama kirusi cha corona kutokana na ukarimu na mshikamano wa Wairani katika kukabiliana na uvonjwa huu.
Habari ID: 3472578    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/03/18

TEHRAN (IQNA) - Majeshi ya Yemen yakishirikiana na kamati za Harakati ya Wananchi ya Answarullah yamefanikiwa kudhibiti eneo la Kufal, ambapo kuna kambi kubwa zaidi ya kijeshi ya muungano vamizi wa Saudi Arabia katika mkoa wa Ma'rib, katikati mwa nchi hiyo.
Habari ID: 3472577    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/03/18

TEHRAN (IQNA)- Mwanazuoni wa ngazi za juu kabisa wa Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Iraq, Ayatullah Sayyid Ali al-Sistani amesema madaktari na wauguzi ambao wanawatibu wagonjwa wa COVID-19 au kirusi cha corona na kisha wanapoteza maisha baada ya kuambukizwa kirusi hicho wakiwa kazini watahesabiwa kuwa ni mashahidi.
Habari ID: 3472576    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/03/17

TEHRAN (IQNA) – Mafunzo ya kuhifadhi Qur’ani Tukufu katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) yatafanyika kwa njia ya intaneti baada ya misikiti na vituo vya Kiislamu kufungwa nchini humo kutokana na hofu ya kuenea ugonjwa wa COVID-19 au corona.
Habari ID: 3472575    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/03/17

TEHRAN (IQNA) – Harakati zote misikitini nchini Malayasia, ikiwa ni pamoja na sala za Ijumaa, zimesitishwa kwa muda wa siku kumi kufuatiia amri ya mfalme wa nchi hiyo ili kuzuia kuenea ugonjwa wa COVID-19 maarufu kama kirusi cha corona.
Habari ID: 3472574    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/03/17