TEHRAN (IQNA) - Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoa taarifa kuhusu makubaliano yaliyotiwa saini jana Jumamosi baina ya Marekani na kundi la Taliban la Afghanistan na kusisitiza kuwa, amani ya kudumu nchini humo itapatikana tu kupitia mazungumzo ya Waafghani wenyewe kwa wenyewe na kushirikishwa makundi yote likiwemo la Taliban.
Habari ID: 3472520 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/03/01
TEHRAN (IQNA) – Serikali ya Afghanistan imesema haina mpango wa kuwaachia huru wafungwa 5,000 wa kundi la Taliban pamoja na kuwa nukta hiyo imetajwa katika mapatano ya Marekani na wanamgambo wa Taliban.
Habari ID: 3472518 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/03/01
TEHRAN (IQNA)- Watu wa Marekani wenye asili ya India wameandamana katika miji mikubwa ya Marekani kulaani mauaji ya makumi katika ghasia za kupinga sheria mpya ya uraia nchini India.
Habari ID: 3472517 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/03/01
TEHRAN (IQNA) - Mfalme wa Malaysia amemteua Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani wa nchi hiyo, Muhyiddin Yassin kuwa Waziri Mkuu mpya, kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Mahathir Muhammad, ambaye alijiuzulu hivi karibuni.
Habari ID: 3472516 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/29
TEHRAN (IQNA) – Vituo vya kufunza Qur'ani Tukufu nchini Kuwait vimefungwa kwa kuhofia kuenea kirusi cha Corona.
Habari ID: 3472515 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/29
Malefu ya Wapalestina washiriki katika Sala ya Ijumaa Msikiti wa Al Aqsa
TEHRAN (IQNA) - Maelfu ya Wapalestina walishiriki katika Salatul Fajr katika Msikiti wa Al Aqsa mjini Quds (Jerusalem) Ijumaa asubuhi licha ya vizuizui vikali vilivyokuwa vimewekwa na jeshi la utawala wa Kizyauni wa Israel.
Habari ID: 3472514 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/29
TEHRAN (IQNA) – Mashindano ya 37 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yanatazamiwa kuakhirishwa kutokana na hofu ya kirusi cha Corona.
Habari ID: 3472513 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/27
TEHRAN (IQNA)- Saudi Arabia imetangaza kusimamisha kwa muda Ibada ya Umrah na Ziyarah katika Msikiti wa Mtume Muhammad SAW mjini Madina kutokana na hofu ya kuenea kirusi cha Corona.
Habari ID: 3472512 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/27
TEHRAN (IQNA) - Idadi ya watu waliouawa katika ghasia zinazosababishwa na sheria tata yenye kuwabagua Waislamu katika mji mkuu wa India, New Delhi inazidi kuongeza ambapo takwimu mpya zinaonyesha kuwa, idadi hiyo imefikia 30 huku mamia ya watu wengine wakijeruhiwa.
Habari ID: 3472511 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/27
Rais Hassan Rouhani
TEHRAN (IQNA) - Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu amesema kuwa Iran imejitayarisha kikamilifu kwa ajili ya kupambana na virusi vya Corona na kwamba mahospitali yote hapa nchini yana vifaa vya kutosha vya kukabiliana na virusi hivyo.
Habari ID: 3472508 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/26
TEHRAN (IQNA) – Msikiti umeteketezwa moto Jumanne katika mtaa wa Ashok Vihar katika mji mkuu wa India, New Delhi huku maandamano ya kupinga sheria mpya ya uraia yakiendelea.
Habari ID: 3472507 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/26
TEHRAN (IQNA) – Kituo kipya cha kuchapisha Qur'ani Tukufu kitafunguliwa katika wilaya ya Sabhan mkoani Mubarak al-Kabeer.
Habari ID: 3472506 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/26
TEHRAN (IQNA) -Rais wa zamani wa Misri, dikteta Hosni Mubarak amefariki dunia hospitalini jijini Cairo akiwa na miaka 91.
Habari ID: 3472505 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/25
TEHRAN (IQNA) - Siku kama ya leo miaka 26 iliyopita, February 25, 1994, Mzayuni mmoja aliyekuwa na misimamo ya kufurutu ada aliwashambulia na kuwamiminia risasi Waislamu waliokuwa wakitekeleza ibada ya Swala katika Msikiti wa Haram ya Nabii Ibrahim mjini al Khalil (Hebron), Palestina inayokaliwa kwa mabavu na kuua shahidi 29 miongoni mwao.
Habari ID: 3472504 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/25
TEHRAN (IQNA) - Mahakama ya Nigeria imeakhirisha tena kusikiliza kesi ya Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria (IMN), Sheikh Ibrahim Zakzaky hadi mwezi Aprili.
Habari ID: 3472503 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/25
TEHRAN (IQNA) - Jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel jana Jumapili lilishambulia kwa mizinga eneo la Ukanda wa Ghaza na kumuua shahidi kijana wa Kipalestina, Mohammed Ali al-Naim aliyekuwa na umri wa miaka 27.
Habari ID: 3472502 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/24
TEHRAN (IQNA)- Waziri Mkuu wa Malaysia Mahathir Mohamad amejiuzulu wadhifa huo. Hatua hiyo ya Mahathir Mohamad inatayarisha uwanja wa kuundwa serikali mpya nchini Malaysia.
Habari ID: 3472501 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/24
TEHRAN (IQNA)- Wataalamu Wairani wamefanikiwa kuunda kifaa maalumu (test kit( cha kupima kirusi cha Corona. Kifaa hicho ni cha kwanza cha aina hiyo kuundwa nchini Iran.
Habari ID: 3472500 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/24
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amewashukuru wananchi kwa kuufuzu kwa kiwango cha kuridhisha mtihani mkubwa wa uchaguzi na kuweza kuzima propaganda za kila upande za maadui na kutumia kwao vibaya suala hilo na akasisitiza kwamba: Taifa zima linapaswa kuwa macho na kujiweka tayari kukabiliana na njama za adui zinazolenga kutoa pigo kwa mihimili tofauti ya nchi.
Habari ID: 3472499 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/23
Imam wa Ahlul Sunna mjini Zahedan, Iran
TEHRAN (IQNA) - Imam wa Ahul Sunna katika mji wa Zahedan, kusini mashariki mwa Iran ameashiria kuenea virusi vya Corona na kusema Mtume Muhammad SAW alitoa nasaha kuhusu namna ya kukabiliana na magonjwa ambukizi ya tauni na kipindupindu.
Habari ID: 3472498 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/23