israel - Ukurasa 5

IQNA

IQNA-Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon, Sheikh Naim Qassem, ametuma salamu za rambirambi kwa taifa la Yemen kufuatia kuuawa shahidi kwa Waziri Mkuu wa Yemen, Ahmad Ghaleb Al-Rahawi, pamoja na mawaziri kadhaa wa serikali yake katika shambulio la anga la Israel lililofanyika hivi karibuni mjini Sanaa.
Habari ID: 3481169   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/01

IQNA-Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pamoja na Spika wa Bunge, Mohammad Baqer Qalibaf, wamelaani vikali hujuma ya hivi karibuni ya kijeshi iliyofanywa na Israel dhidi ya Yemen, ambayo imesababisha kuuawa kwa shahidi Waziri Mkuu wa Yemen na mawaziri kadhaa wa serikali ya mapinduzi ya nchi hiyo.
Habari ID: 3481163   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/31

IQNA – Mkutano wa dharura wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wa Shirika la Ushirikiano la Kiislamu (OIC) ulianza Jumatatu mjini Jeddah, Saudi Arabia, ambapo washiriki wamesisitiza umuhimu wa hatua ya pamoja kusaidia Gaza na Palestina.
Habari ID: 3481136   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/26

IQNA – Kamati za Upinzani za Kawaida (PRC), muungano wa makundi ya Kipalestina, zimelaani mashambulizi ya kijeshi ya utawala wa Israel yaliyolenga miundombinu nchini Yemen.
Habari ID: 3481132   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/25

IQNA- Maandamano yafanyika Uingereza kulaani  mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na Israel dhidi ya Gaza Maandamano makubwa yamefanyika nje ya ubalozi wa utawala wa Israel mjini London, Uingereza kulaani mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na utawala huo dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.
Habari ID: 3481127   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/24

IQNA – Watu wa Yemen katika mkoa wa Saada wameshiriki katika maandamano ya mamilioni ya watu Ijumaa, wakionesha mshikamano wao na watu wanaodhulumiwa Palestina hasa katika Ukanda wa Gaza.
Habari ID: 3481124   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/23

IQNA-Mshambuliaji wa timu ya soka ya Liverpool, Mohamed Salah amekosoa hatua ya Muungano wa Vyama vya Soka vya Ulaya UEFA ya kumuenzi Suleiman Al-Obeid, anayejulikana kama "Pele wa Palestina," baada ya bodi inayosimamia soka ya Ulaya kutoelezea mazingira ya kifo chake wiki hii.
Habari ID: 3481065   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/10

IQNA – Shirika moja la utetezi wa haki limeshutumu agizo jipya kutoka kwa serikali ya Trump linalozuia utoaji wa misaada ya majanga kwa majimbo na miji ya Marekani inayopinga bidhaa na makampuni ya Israel yanayoshiriki katika uhalifu wa kivita, likilitaja kuwa si la kizalendo, linakiuka katiba, na ni shambulio dhidi ya haki za binadamu na uhuru wa kujieleza.
Habari ID: 3481048   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/07

IQNA – Mkurugenzi wa Msafara wa Hijja wa Iran ameifu mshikamano wa kimataifa uliodhihirika wakati wa vita vya siku kumi na mbili vilivyoanzishwa na utawala wa Israel dhidi ya Iran, na ametilia mkazo umuhimu wa umoja wa Waislamu kuelekea Siku ya Arbaeen ya Imam Hussein (AS).
Habari ID: 3481035   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/04

IQNA – Picha zilizopigwa mwishoni mwa Julai 2025 zinaonesha athari za mashambulizi ya kigaidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya mji mkuu wa Iran, Tehran, mwezi Juni, ambapo maeneo ya makaazi ya raia yalilengwa.
Habari ID: 3481033   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/02

IQNA-Katibu Mkuu wa Hizbullah nchini Lebanon, amesisitiza kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel na Marekani wanatekeleza jinai za kila siku, zilizo na mpangilio mahsusi, katika Ukanda wa Gaza.
Habari ID: 3481023   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/31

IQNA – Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatعllah Sayyid Ali Khamenei, amesema kuwa vita vya siku 12 vilivyoanzishwa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran vimeonesha kwa dhahiri uimara wa kipekee wa Jamhuri ya Kiislamu pamoja na dhamira thabiti na uwezo wake mkubwa.
Habari ID: 3481016   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/29

IQNA-Sheikh Muhammad Ahmad Hussein, Mufti Mkuu wa Al-Quds, amepigwa marufuku na utawala dhalimu wa Israel kuingia Msikiti wa Al-Aqsa ulio mjini Quds (Jerusalem) kwa muda wa wiki moja, marufuku ambayo inaweza kuongezwa
Habari ID: 3481015   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/28

IQNA-Jeshi la majini la utawala ghasibu wa Israel limeiteka meli ya misaada iliyokuwa ikielekea Ukanda wa Gaza, ikiwa na bendera ya Uingereza, katika harakati za kuvunja mzingiro mkali wa eneo hilo unaoendelea tangu mwaka 2007.
Habari ID: 3481010   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/27

IQNA – Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kwamba mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran yameshindwa kutimiza malengo waliyojiwekea, huku akisisitiza kwamba taifa hilo litaendelea kusonga mbele kwa kasi zaidi katika nyanja za kijeshi na kielimu kwa azma iliyo imara.
Habari ID: 3481003   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/26

IQNA-Kiongozi mkuu Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Iraq, Ayatullah Sayyid Ali al-Sistani, ameelezea masikitiko yake makubwa kuhusu hali ya kibinadamu inayoendelea kuzorota katika Ukanda wa Gaza, hususan baa la njaa linalozidi kushika kasi, na kutoa wito kwa mataifa ya Kiarabu na Kiislamu kuchukua hatua za haraka kukomesha janga hili la kusikitisha.
Habari ID: 3481002   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/26

IQNA-Mmoja wa viongozi wa ngazi za juu kidini nchini Iran amemwandikia barua Papa Leo XIV akisema: "Mienendo ya kikatili na isiyo ya kibinadamu ya utawala wa Kizayuni wa Israel ikiwa ni pamoja na kuzuia kupelekwa chakula na mahitaji muhimu kwa watu wa Gaza ni ukiukaji wa wazi wa kanuni za kidini, kibinadamu, maadili na sheria za kimataifa."
Habari ID: 3480994   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/25

IQNA – Mwanazuoni wa ngazi za juu wa Kiislamu kutoka Iran amewataka viongozi wa Kiislamu na Kiongozi wa Kanisa Katoliki kushikamana dhidi ya mzingiro wa Israel huko Gaza, ambako njaa inazidi kupelekea janga kubwa la kibinadamu.
Habari ID: 3480992   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/24

IQNA – Sheikh Ahmed al-Tayeb, Imamu Mkuu wa Al-Azhar, ametoaito wa dharura kwa jamii ya kimataifa kuingilia kati mara moja kuokoa watu wa Gaza dhidi ya baa la njaa linalokatili maisha ya wengi.
Habari ID: 3480989   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/23

IQNA – Profesa Ali Montazeri, Mkuu wa Akademia ya Kitaifa cha Elimu, Utamaduni na Utafiti (ACECR) nchini Iran, amesema kuwa lengo la mashambulizi ya pamoja ya Marekani na Israel dhidi ya Iran ni kuzuia maendeleo ya kisayansi na kiteknolojia ya taifa hilo.
Habari ID: 3480977   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/21