"Haipaswi kuwa na shaka kwamba kile kilichotokea nchini Syria kilipangwa katika vyumba vya kamandi vya Marekani na Israel. Tuna ushahidi wa hili," Ayatullah Khamenei aliambia kundi la watu huko Tehran Jumatano.
"Moja ya nchi jirani za Syria pia ilikuwa na nafasi katika hilo, lakini wapangaji wakuu ni Marekani na utawala wa Kizayuni," Kiongozi Muadhamu alisema.
Ayatullah Khamenei alibatilisha uvumi kuhusu kudhoofika kwa safu ya muqawama au mapambano ya Kiislamu baada ya wanamgambo na magaidi wa kitakfiri kuuvamia mji mkuu wa Syria, huku akitoa hakikisho kuwa muqawama utaimarika zaidi.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuhusiana na muqawama kwamba, harakati na muqawama wa wananchi utaenea katika eneo lote la Asia Magharibii kuliko ilivyokuwa hapo kabla.
Ayatullah Khamenei amesema: "Kadiri muqawama uunavyoshinikizwa ndivyo unavyoimarika zaidi, kadiri maadui wanavyotenda jinai ndivyo muqawama unavyokkuwa na msukumo na azma zaidi na kadiri kunavyoendeshwa vita dhidi yake ndivyo unavyopanuka na kuenea zaidi. Wachambuzi wasio na uelewa ambao hawafahamu maana ya Muqawama wanadhani kuwa iwapo muqawama utadhoofika, Iran ya Kiislamu nayo itadhoofika. Nasema hapa kwamba, kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu, Iran ina inguvu na itakuwa na nguvu zaidi."
Kadhalika Ayatullah Khamenei amesema: "Mimi nawaambia kwamba, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, muqawama na mapambano yataenea katika eneo lote la Asia Magharibi kuliko ilivyokuwa hapo kabla."
Kuhusiana na mwenendo wa utawala wa Syria wa kutotilia maanani tahadhari zilizotolewa kuhusu hali ya ndani ya nchi hiyo. Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: "Tangu miezi kadhaa iliyopita shirika letu la upelelezi lilituma ripoti za tahadhari kwa viongozi wa Syria, sijui ikiwa ziliwafikia viongozi wakuu au zilipotea katikati. Lakini maafisa wetu wa upelelezi waliwatahadharisha katika ripoti kadha tangu miezi kadhaa iliyopita."
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria kadhia ya fitna ya magaidi wa Daesh na kusema: "Daesh yaani bomu la ukosefu wa usalama, Daesh maana yake ilikuwa ni kuivuruga Iraq, kuiyumbisha Syria, kuyumbisha eneo hili, kisha kuja kwenye nukta kuu na lengo la mwisho, ambalo ni Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kuiyumbisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Hili lilikuwa lengo kuu na la mwisho. Hii ndio maana ya Daesh."
Kiongozi Muadhamu akiashiria kuhusu ardhi za Syria ambazo zinakaliwa kwa mabavu amesema: "Maeneo yanayokaliwa kwa mabavu ya Syria yatakombolewa na vijana wenye bidii wa Syria. Msiwe na shaka kuwa haya yatatokea. Satwa Marekani pia haitakuwa na nguvu. Kwa neema na uwezo wa Mwenyezi Mungu, Marekani pia itafukuzwa katika eneo hilo kwa jitihada za Muqawama."