IQNA

Samoa yataka kuupiga marufuku Uislamu

13:59 - May 25, 2016
Habari ID: 3470335
Kiongozi wa Kikristo nchini Samoa ameitaka serikali ya nchi hiyo ya Bahari ya Pasifiki kuupiga marufuku Uislamu.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Kasisi Ma'auga Motu, Katibu Mkuu wa Baraza la Makanisa ya Samoa anaishinikiza serikali ya nchi hiyo kupiga marufuku Uislamu katika visiwa.

Waziri Mkuu wa nchi hiyo Tuilaepa Sailele Malielegaoi wiki iliyopita alitoa wiot wa kufanyiwa marekebisho vipengee vya uhuru wa kuabdudu katika Katiba ya Samoa.

Alisema analenga kuhakikisha itikadi za Kikristo zinaingizwa kikamilifu katika katiba hiyo.

Kwa msingi huo Kasisi Motu amemtaka waziri mkuu kusonga mbele zaidi na kuupiga marufu Uislamu ambao amedai ni tishio kwa mustakabali ya nchi hiyo.

Amebainisha wasi wasi wake kuhusu kuongezeka idadi ya watu wanaovutiwa na Uislamu nchini humo na hivyo kuwafanya Waislamu wawe na ushawishi.

Katika kujibu matamshi hayo ya chuki dhidi ya Uislamu, Imamu Mkuu wa Samoa amesema Wakristo katika kisiwa hicho wanapaswa kuvumilia dini nyinginezo na kuacha vitendo vya ubaguzi.

Imam Mohammad bin Yahya amesema Samoa inaweza kupata matatizo ya kufanya biashara na nchi za Kiislami iwapo katiba ya nchi hiyo itabadilishwa. Katika sense ya mwaka 2001, ilibainika kuwa asilimia 0.03 ya wakaazi wote wa visiwa ni Waislamu huku waliowengi wakiwa ni Wakristo.

Samoa ni nchi iliyo katika Bahari ya Pasifiki inayojumuisha visiwa viwili vikuu vya Savai'I na Upolu na visiwa vingine vine vidogo. Mji wake mkuu ni Apia huku ikiwa na idadi ya watu wake ikikadiriwa kuwa 190,000.

3500947

captcha