IQNA

Mwanamke wa kwanza Mwislamu kuchaguliwa kugombea ubunge Minnesota, Marekani

7:58 - August 16, 2016
Habari ID: 3470525
Mwanamke Mwislamu Mmarekani, Ilhan Omar ameweka historia kwa kuchaguliwa kugombea kiti katika Bunge la Wilaya ya 60B jimbo la Minnesota nchini Marekani.

Akizungumza baada ya matokeo ya uchaguzi huo wa mchujo wa Agosti 6, Ilan Omar wa chama cha Democrat na mwenye asili ya Somalia alisema. "Leo tumeandika historia. Leo ni mwanza wa mustakabali mpya wa wilaya yetu.”

Ilhan Omar mwenye umri wa miaka 33 alizaliwa Somalia kabla ya kukimbilia Marekani kutokana na vita katika nchi yake.

Alipokimbia Somalia awali aliishi kwa muda wa miaka mine katika kambi ya wakimbizi nchini Kenya kabla ya kuelekea Marekani katika eneo lenye Wasomali wengi la Cedar-Riverside ambapo aliishi kwa miongo miwili na sasa ni mkurugenzi wa Jumuiya ya Kuwaleta Pamoja Wanawake.

Omar amemshukuru baba yake, mume na watoto wake pamoja na hayati babu yake kwa kumfundihsa kuhusu demokrasia.

Mwezi Novembe Omar atachuana na Abdimali Askar wa chama cha Republican katika uchaguzi wa kuwakilisha eneo hilo katika bunge la kieneo.

3460692

captcha