IQNA

Mashindano ya Kitaifa ya Qur’ani Iran kufanyika

19:24 - September 27, 2020
Habari ID: 3473207
TEHRAN (IQNA) – Mkuu wa Idara ya Masuala ya Qur’ani katika Shirika la Wakfu la Iran amesema mashindano ya kitaifa ya Qur’ani nchini Iran mwaka huu yatafanyika kwa njia ya intaneti.

Mehdi Qarasheikhlu amesema mashindano hayo yalikuwa yafanyike katika ukumbi lakini kutokana na kuongezeka maambukizi ya corona katika siku za hivi karibuni, imeamuliwa yafanyika kwa njia ya intaneti.

Amesema mchujo wa mashindano umekamilika katika mikoa 31 kote Iran na fainali za kitaifa zitafanyika mwezi ujao. Mashindano hayo ya kila mwaka huwashirikisha mabingwa kutoka kote Iran ambapo vipaji vipya huweza kubainika.

3925533

captcha