Uchambuzi huu umetolewa na Sheikh Ali Al-Fatlawi, mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Warith Al-Anbiya, Karbala, ambaye katika makala yake amebainisha siri ya kubaki hai kwa harakati ya Husseini na taathira yake katika dhamiri ya umma. Hii hapa sehemu ya uchambuzi huo
Tofauti ya Kimsingi: Kati ya ‘Nahdha’ na ‘Inghilabu’
Kabla ya kuzama katika misingi iliyofanya harakati hii kutofutika, ni lazima tufafanue dhana mbili muhimu: Nahdha (Mwamko/Harakati) na Inqilab (Mapinduzi).
Harakati ya Ashura inajumuisha dhana zote mbili. Ni Inqilab kwa sababu ilikuwa ni uasi dhidi ya mfumo wa kitaghoot (dhalimu) na fisadi, lakini ni Nahdha kwa sababu ilikuwa na malengo ya kuelekea kwenye ukamilifu wa kibinadamu na uadilifu.
Nguzo za Kudumu kwa Harakati ya Imam Hussein (AS)
Licha ya kutokea kwa harakati nyingi kabla na baada ya Karbala, hakuna iliyofikia hadhi, heshima, na kugeuka kigezo cha kudumu kama mwamko wa Bwana wa Mashahidi, Imam Hussein (AS). Ashura ni kilele cha maadili yote ya kijeshi, kidini, na kisaikolojia.
Siri ya kubaki kwa harakati hii inategemea nguzo nne:
1. Misingi ya Kiungu (Rabbaniyyah):
Imam Hussein (AS) hakutafuta mamlaka ya kidunia, bali alitekeleza ahadi ya Mwenyezi Mungu ya kunusuru neno Lake. Kama isemavyo Qur’ani: “Yeye ndiye Aliyemtuma Mtume Wake kwa uongofu na Dini ya Haki…” (Al-Fath: 28). Ushindi wa Imam Hussein si wa kijeshi pekee, bali ni ushindi wa kifikra ambapo harakati yake imebaki kuwa mnara wa uongofu (Misbahul-Huda).
2. Shakhsia ya Kiongozi:
Hussein (AS) ni Imam maasum, aliyehitimu sifa zote za ukamilifu: uchamungu, ushujaa, elimu, na kujiweka mbali na dunia (zuhd). Kama alivyosema Mtume (SAW): “Hassan na Hussein ni Maimamu, wawe wamesimama au wamekaa (kufanya suluhu au vita).”
3. Mipango Makini (Tadh-hiyah):
Mafanikio ya Karbala hayakuwa ya bahati mbaya. Mtume (SAW) alikuwa ameshaandaa mazingira ya kisaikolojia kwa kutabiri mauaji ya mjukuu wake ili umma utambue haki. Imam Hussein (AS) naye alipanga muda wa mwamko wake na kuchagua masahaba wake kwa umakini mkubwa.
4. Jukumu la Kibalagha na Uenezi (Media):
Baada ya mauaji ya Karbala, jukumu la kuhuisha damu hiyo lilibebwa na Imam Zayn al-Abidin (AS) na Bibi Zaynab al-Kubra (SA). Hotuba zao zenye ufasaha mbele ya madhalimu ziliifanya damu ya mashahidi isipotee na kuifikisha sauti ya haki kila kona ya ulimwengu.
Malengo Matukufu na Athari zake
Imam Hussein (AS) aliweka wazi malengo yake kupitia kauli na msimamo wake:
Hitimisho la Kimafunzo
Kutokana na harakati hii, tunajifunza misingi muhimu kwa vizazi vyote:
1.Kukataa serikali yoyote isiyo na uhalali wa kisheria na kimaadili.
2..Kutonyamazia dhuluma, kwani kunyamaza ni kuipalilia dhuluma hiyo.
3..Kujitolea kitu chenye thamani zaidi (nafsi na mali) kwa ajili ya kulinda Dini.
4. Kiongozi wa kweli lazima apambike na uaminifu, uchamungu, na usafi wa kiroho.
Harakati ya Ashura inabaki kuwa shule ya kudumu ya ukombozi, ikitufundisha kuwa haki haishindwi na upanga, na kwamba damu ya mwenye kudhulumiwa ina nguvu kuliko majeshi ya dhalimu.
4360209