Kwa mujibu wa Idara ya Wakfu ya Kiislamu inayoendeshwa na Jordan, ambayo inasimamia masuala ya Msikiti wa al-Aqsa, takriban walowezi 1,390 walikiuka utakatifu wa eneo hilo kupitia lango la Morocco, ambalo pia linajulikana kama lango la Mughrabi.
Walioshuhudia waliripoti kwamba waziri mwewe wa Israel Itamar Ben-Gvir alijiunga na walowezi katika kutekeleza matambiko ya Talmudi kwenye eneo takatifu.
Maafisa wa Israel na walowezi mara kwa mara huvamia eneo la Msikiti wa al-Aqsa, jambo ambalo huzua hisia kali kutoka kwa Wapalestina na mataifa mengine ya Kiislamu. Ziara hizo za uchochezi kwa kawaida hupangwa na vikundi vya mahekalu vinavyoungwa mkono na Tel Aviv na hufanyika chini ya usimamizi wa vikosi vya jeshi la Israel huko al-Quds.
Kiwanja cha Msikiti wa al-Aqsa, kilicho juu ya plaza ya Ukuta wa Magharibi, kinajumuisha Al Qubbat Sakhra na Msikiti wa al-Aqsa. Ingawa kutembelea kwa Wayahudi al-Aqsa kunaruhusiwa, makubaliano ya muda mrefu kati ya Jordan na Israel, yaliyoanzishwa baada ya Israel kuikalia kwa mabavu al-Quds Mashariki mwaka 1967, yanapiga marufuku ibada ya wasio Waislamu kwenye eneo hilo.
Mataifa kadhaa ya kikanda, ikiwa ni pamoja na Iran, Jordan, na Qatar, yalipinga ukiukaji wa hivi karibuni wa Israeli wa eneo hilo takatifu ya Waislamu.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Esmaeil Baghaei amelaani jinai za Israel huko Gaza na ukiukaji wa utakatifu msikiti wa al-Aqsa katika taarifa ya Jumapili.
Wizara ya Mambo ya Nje na Wageni ya Jordan ilisema shambulio hilo ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa, hadhi ya kihistoria na kisheria iliyopo Quds na maeneo yake matakatifu, na wajibu wa Israel kama "utawala ghasibu," kulingana na taarifa ya wizara hiyo.
Msemaji wa wizara hiyo Sufian Qudah amesema kuwa Israel lazima ikomeshe ukiukaji na ukiukaji wote unaoendelea wa kihistoria na kisheria uliopo Quds Tukufu na maeneo yake matakatifu, akitaka kukomeshwa kuwekewa ukweli mpya katika Msikiti wa al-Aqsa.
Wakati huo huo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar ililaani uchochezi wa hivi punde katika taarifa ya Jumapili. Doha ilionya juu ya madhara ya majaribio ya mara kwa mara ya Israel ya kuhatarisha hadhi ya kidini na kihistoria ya Msikiti wa Al-Aqsa. Imesisitiza kuwa jumuiya ya kimataifa inapaswa kubeba wajibu wake wa kimaadili na kisheria kuhusu mji wa Quds na maeneo yake matakatifu.
Hayo yanajiri huku utawala haramu wa Israel ukiendeleza mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza, ambayo yamesababisha vifo vya Wapalestina wasiopungua 42,603, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, tangu Oktoba 7 mwaka jana.
3490362