IQNA

Jinai

Hujuma ya Marekani na Uingereza dhidi ya Harakati ya Ansarullah ya Yemen

21:46 - December 17, 2024
Habari ID: 3479914
IQNA-Siku moja baada ya vikosi vya ulinzi vya Yemen kushambulia mji mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel Tel Aviv kwa kombora la 'hypersonic, la Palestina 2 ndege za kivita za Marekani na Uingereza zimeshambulia maeneo kadhaa ya Harakati ya Ansarullah katika mji mkuu wa Yemen, Sana'a

Mashambulizi hayo ya anga dhidi ya Sana'a na Hodeidah nchini Yemen yameongozwa na Marekani na kueleza kuwa, jengo la vikosi vya ulinzi vya Yemen lililengwa katika shambulio hilo.

Wakati huo huo, redio ya Jeshi la Kizayuni ikinukuu Kamandi Kuu ya Jeshi la Marekani imetangaza kuwa, kamandi hiyo imefanya mashambulizi ya anga dhidi ya kituo cha kamandi na usimamizi cha jeshi la Yemen mjini Sana'a.

Mashambulio ya anga ya Marekani na Uingereza yamefanywa kufuatia shambulio la kombora la 'hypersonc' aina ya Palestina 2 lililofanywa na Yemen jana usiku.

Kufuatia shambulio hilo, baadhi ya vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni vimetangaza kufanyika kikao cha dharura cha maafisa wa kijeshi na kisiasa wa utawala huo kwa ajili ya kupanga mashambulizi dhidi ya Sana'a.

Hapo awali jeshi la Yemen lilitangaza katika taarifa lililotoa jana usiku kwamba vikosi vya jeshi la nchi hiyo vimeshambulia eneo la Jaffa kaskazini mwa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) kwa kutumia kombora la 'hypersonic' la "Palestina 2" na kwamba operesheni hiyo ilifanikiwa kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Vikosi vya ulinzi vya Yemen vimesisitiza kuwa, vitaendeleza operesheni zake za kijeshi na kushambulia maeneo yote ya adui Mzayuni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu; na operesheni hizo hazitasitishwa hadi pale mashambulizi ya jeshi la utawala ghasibu wa Israel dhidi ya Ghaza yatakapokomeshwa na mzingiro wake kuondolewa.

4254653

Habari zinazohusiana
captcha