Meli hiyo, Galaxy Leader, inayomilikiwa na mfanyabiashara Muisrali, ilikamatwa na wanajeshi wa Yemen katika Bahari ya Sham kama njia ya kuonyesha mshikamano na Wapalestina madhulumu wa Ukanda wa Gaza, ambao wamekuwa wakikabiliwa na vita vya mauaji ya kimbari vya utawala wa Kizayuni wa Israel kwa takriban mwaka mmoja.
Picha na video zilizosambazwaa na Ansarullah kupitia Televisheni ya Al Masirah zinaonyesha meli hiyo ikiwa imepambwa kwa taa za kijani.
Tukio hilo limejiri wakati miji kote Yemen imepambwa kwa mnasaba sherehe za Milad-un-Nabi.
Meli ya kibiashara ya Galaxy Leader ilikamatwa na wanajeshi wa Yemen katika Bahari Sham mnamo Novemba 20, 2023.
Wafanyakazi 25 wa meli hiyo pia wanazuiliwa na vikosi vya Yemen.
Hapo nyuma, Ansarullah ilitoa picha zinazoonyesha vikosi vyake vikishuka kutoka kwenye helikopta ya kijeshi hadi kwenye sitaha ya meli ya hiyo Israel katika operesheni maalumu ya kuzuia Bahari ya Sham kutumiwa kuifikishia Israel bidhaa muhimu.
Utawala wa Israel ulidai kuwa meli hiyo si yake lakini ushahidi wa baadaye ulithibitisha kuwa utawala huo unahadaa kuepuka fedheha.
Tangu tarehe 7 Oktoba, wakati utawala wa Israel ulipoanzisha vita vyake dhidi ya Ukanda wa Gaza, vikosi vya jeshi la Yemen vimeendesha operesheni kadhaa dhidi ya meli za kibiashara za utawala haramu wa Israel kama njia ya kuwaunga mkono Wapalestina. Aidha majeshi ya Yemen yametekeleza operesheni kadhaa za makombora dhidi ya ngome za utawala wa Kizayuni wa Israel.
4236481