IQNA

22:29 - May 10, 2022
Habari ID: 3475231
TEHRAN (IQNA)- Mashindano ya Qur’ani kupitia mitandao ya kijamii yamefanyika nchini Tanzania kwa himya ya Kituo cha Utamaduni cha Iran mjini Dar es Salaam ambapo washindi wametunukiwa zawadi.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, katika Mwezi Mtukufu  wa Ramadhani, Kituo cha Utamaduni cha Iran mjini Dar es Salaam kiliandaa mashindano ya Qur’ani kwa njia ya mitandao ya kijamii.

Katika mashindano hayo, washiriki walitakiwa kutuma klipu fupi za qiraa yao ya Qur’ani Tukufu na kutuma katika ukurasa wa Kituo cha Utamaduni cha Iran.

Katika mashindano hayo washiriki wanne ambao klipu zao zilitembelewa na watu wengi zaidi wametunukiwa zawadi.

Washindi wa mashindano hayo walikuwa ni pamoja na Yassin Mohammad Haruna, Ali Mohammad, Mustafa Mkunga na Mohammad Abdalla Mkadam.

4055758

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: