Hujjatul Islam wal Muslimin Hamid Shahriyari ameuambia mkutano wa Umoja wa Kiislamu uliofanyika mjini Islamabad Pakistan kwamba, Waislamu wanapaswa kuzika hitilafu zao, kwani siri ya mafanikio yao ni kujiepusha na uchochezi wa hitilafu na migawanyiko.
Shahriyari ameongeza kuwa, Waislamu wanaweza kuunda muungano wa nchi za Waislamu kwa utangamano, mshikamano na kujiepusha na makabiliano.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu amesema, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imefanya jitihada kubwa sana kwa ajili ya kupanua na kuimarisha zaidi umoja na mshikamano baina ha Waislamu.
Balozi wa Iran nchini Pakistan, Sayyid Muhammad Hosseini pia alihutubia mkutano huo ambapo amelaani hujuma na propaganda chafu dhidi ya Uislamu na kusema, umoja na juhudi za kukururbisha pamoja madhehebu za Kiislamu ni mambo mawili muhimu ya uokovu wa Umma wa Waislamu mkabala wa njama zinazofanywa na maadui yao.