IQNA

Sura za Qur'ani Tukufu /14

Sura Ibrahim; Sisitizo kuhusu malengo ya pamoja ya Manabii wa Mwenyezi Mungu

14:26 - October 16, 2022
Habari ID: 3475939
TEHRAN (IQNA) – Aya za Sura Ibrahim zinataja utume wa Mitume wa Mwenyezi Mungu bila ya kutaja mahususi kwa mtume au watu fulani.

Kwa hivyo inaweza kusemwa kwamba manabii wote wa Mwenyezi Mungu wamefuata njia moja na wote wamefanya jitihada za kuwaongoza watu kwa mpango wa pamoja.

Sura Ibrahim ni sura ya 14 ya Quran. Imepewa jina la Nabii Ibrahim (Ibrahim), ni sura ya Makki (iliyoteremshwa Makka) ambayo ina aya 52 na iko katika Juzuu ya 13 ya Qur'ani Tukufu. Ni Sura ya 72 aliyoteremshiwa Mtume Muhammad (SAW).

Sababu ya Sura hii kuitwa Ibrahim (AS) ni kwa sababu inasimulia kisa cha Mtume huyu mkubwa. Nabii Ibrahim (AS) ametambulishwa katika Sura hii kwa maombi yake. Ni sura ya pekee ya Quran ambayo Nabii Ibrahim (AS) anakumbukwa kwa maombi au dua yake, ambayo ni miongoni mwa dua zilizotajwa ndani ya Quran.

Katika sura hii, kuna mijadala mingi kuhusu imani na misingi ya kiitikadi na amri pekee iliyo nayo kwa waumini ni kuwaamrisha kusali na kufanya Infaq (kutoa sadaka) kwa siri na kwa uwazi.

Masuala makuu yaliyojadiliwa katika Sura ya Ibrahim ni Tauhidi, Siku ya Kiyama na tathmini ya matendo ya mwanadamu siku hiyo. Allamah Tabatabai mfasiri maarufu wa Qur'ani Tukufu aliyeandika Tafsir al Mizan anaichukulia ufafanuzi kuhusu Qur'ani Tukufu kuwa ndio mada kuu katika sura hii, kwa kuwa ni alama ya ujumbe wa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) ambamo anawaokoa watu kutoka gizani na kuwaongoza kwenye nuru na njia ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi.

Miongoni mwa mada nyingine zilizotajwa katika Sura hii ni utume wa Mitume wa Mwenyezi Mungu. Kwa mujibu wa Surah Ibrahim, Mitume wote wa Mwenyezi Mungu walifuata lengo moja. Sehemu kubwa ya Sura, bila ya kumtaja mtume maalum, inahusu mijadala baina ya Mitume na wale waliowapinga. Inabainisha kanuni na misimamo ya jumla ya manabii wa Mwenyezi Mungu na miitikio ya wakanushaji.

Sura Ibrahim pia inaeleza tofauti kati ya nuru na giza, wema na uovu, uthabiti na kutotulia, na uthabiti na kutodumu katika kuwasilisha ripoti kuhusu kisa cha Mitume ambao daima walikuwa wakiwakabili wale waliowakadhibisha na kuwapinga.

3479453

Habari zinazohusiana
captcha