IQNA

Sura za Qur'ani Tukufu /25

Maajabu ya Bahari katika Surah Al-Furqan

22:02 - August 14, 2022
Habari ID: 3475622
TEHRAN (IQNA) – Kuna mahali karibu na Denmark ambapo bahari mbili huunda mandhari ya kuvutia. Eneo moja kuna maji ya chumvi na nyingine maji matamu. Kwa sifa zao tofauti, bahari mbili hazichanganyiki kana kwamba kuna kizuizi kati yao.

Jambo hili la kushangaza limetajwa katika Surah Al-Furqan.

Sura Al-Furqan ni sura ya 25 ya Qur'ani Tukufu. Surah hii nii Makki, ina aya 77 na iko katika Juzuu za 18 na 19 za Qur'ani Tukufu. Ni Sura ya 42 iliyoteremshwa kwa Mtukufu Mtume (SAW).

Furqan maana yake ni kile kinachotenganisha na kutofautisha kati ya ukweli na uwongo. Pia ni moja ya majina ya Qur'ani Tukufu.

Sura ya Al-Furqan inajumuisha mijadala kuhusu Tauhidi (kuamini Mungu Mmoja), Siku ya Kiyama, utume, na kupiga vita ibada ya masanamu. Katika Aya za mwisho, inaeleza kwa kina juu ya sifa za waumini walio imara.

Sura inaweza kugawanywa katika sehemu tatu kulingana na mada:

Katika sehemu ya kwanza inakosoa mantiki ya Mushrikeen (washirikina), inajibu visingizio wanavyotoa vya kutokubali ukweli, na inawaonya kuhusu adhabu ya Mwenyezi Mungu. Kama somo, pia inahusiana na sehemu za hadithi za watu walioishi kabla na kukabiliwa na adhabu kali kwa kuwapinga Mitume wa Mwenyezi Mungu.

Katika sehemu ya pili, ushahidi umetolewa kwa ajili ya Tauhidi na zimetajwa baadhi ya dalili za Mwenyezi Mungu duniani, kuanzia kwenye mwanga wa jua hadi giza la usiku, kupuliza upepo, mvua, kuhuishwa ardhi baada ya kunyesha mvua, kuumbwa kwa mbingu na ardhi katika siku sita na uumbaji wa jua na mwezi na jinsi wanavyotembea katika mzunguko wao wenyewe.

Miongoni mwa masuala yaliyotajwa katika Sura kuwa ni maajabu ya uumbaji ni lile lililo katika Aya ya 53: “Naye ndiye aliye zipeleka bahari mbili, hii tamu mno, na hii ya chumvi chungu. Na akaweka baina yao kinga na kizuizi kizuiacho.”

Aya ya 19 ya Surah Ar-Rahman na aya ya 61 ya Surah An-Naml pia zinazungumzia juu ya bahari mbili. Kwa sifa zilizotajwa katika Qur'ani kuhusu bahari mbili, inaweza kusemwa kwamba inarejelea mahali ambapo Bahari ya Baltic na Bahari ya Kaskazini hukutana karibu na Skagerrak.

Sehemu ya tatu ya Sura Al-Furqan inaeleza kwa kina juu ya sifa za waumini wenye msimamo thabiti na waja wa kweli wa Mwenyezi Mungu kinyume na makafiri ambao daima hutafuta udhuru. Baadhi ya sifa za waumini waliotajwa katika Sura ni pamoja na imani nzuri, matendo mema, kupinga matamanio ya kidunia, kuwa na dhamira na wajibu wa kijamii na kuwa na utambuzi.

3480065

Habari zinazohusiana
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha